29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Kijaji azitaka benki kupunguza gharama za uendeshaji

Na MWANDISHI WETU, DODOMA

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji amezitaka taasisi za fedha nchini kujipanga kikamilifu kukabiliana na suala la mikopo chechefu pamoja na kupunguza gharama za uendeshaji.

Dk Kijaji alitoa changamoto hiyo jana jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa tawi jipya la Benki ya Azania ambapo alisema hali hiyo itazisaidia kuweza kuwahudumia wateja wake kwa gharama za chini zaidi ikilinganishwa na hali ilivyo sasa.

“Chanzo cha mikopo chefu ni watumishi wasio waadilifu kwenye taasisi hizi na ndio maana naomba sana bodi na menejimenti ziwachukulie hatua sambamba na kupunguza gharama za uendeshaji kwa sababu sisi kama serikali hatutavumilia uzembe wa aina yoyote katika utekelezaji wa hili.’’ alisisitiza.

Awali akizungumza kwenye uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Charles Itembe alisema kwa sasa benki hiyo ina matawi 19 likiwamo hilo jipya lililopewa jina la Sokoine, ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa Waziri Mkuu wa zamani,  Hayati Edward Moringe Sokoine.

“Malengo yetu ya kimkakati kwa sasa ni kukuza mtatandao wa matawi ya benki yetu, angalau matawi matatu kwa mwaka na pia kukuza nafasi yetu ya umiliki wa soko angalau kwa asilimia tatu ndani ya miaka mitatu.’’ alisema Itembe.

Alisema nia ya benki hiyo ni kuwa katika hadhi ya mabenki makubwa daraja la kwanza ikizingatiwa Dodoma kuwa jiji kumeiweka benki hiyo katika nafasi nzuri sambamba na mahitaji ya fedha ikizingatiwa kuwa mkoa huo upo katikati ya nchi na ni makao makuu ya serikali.

Benki ya Azania imezidi kujitanua baada ya kuzindua tawi lake jipya jijini Dodoma ikiwa ni muendelezo wa mkakati wa benki hiyo kukuza mtatandao wa matawi yake kwa kuunga mkono jitihada Rais John Magufuli kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda kupitia huduma bora za kibenki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles