23.2 C
Dar es Salaam
Sunday, March 26, 2023

Contact us: [email protected]

Watakaopandisha nauli Krismasi kukiona

Na AVELINE KITOMARY, DAR ES SALAAM 

CHAMA cha Kutetea abiria Tanzania (CHAKUA) kimewataka abiria wanaosafiri kwenda mikoa mbalimbali nchini kuchukua tahadhari kwa kutoa taarifa pale wanapotozwa nauli tofauti na iliyowekwa na Serikali.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mwenyekiti wa chama hicho, Hassan Mchanjama  alisema wanaendelea kutoa elimu na kuwatahadharisha makondakta na madereva ambao watatoza nauli kinyume na utaratibu kuwarudishia abiria kiasi kilichozidi kikiambatana na faini.

“Tahadhari kwa abiria wasikubali kutozwa nauli kubwa wahakikishe wanalipa kiwango kilichowekwa na serikali kama taratibu zikikiukwa watoe taarifa CHAKUA, tumesha dhibiti magari mengi kwa kurudisha nauli na kutozwa faini,”alieleza Mchanjama.

Aidha Mchanjama alisema lengo lao ni kuwatetea abiria kupata haki zao hivyo wanashirikiana na SUMATRA pamoja na Jeshi la Polisi kuyadhibiti na kuyachukulia hatua za sheria mabasi yatakayobainika kupandisha nauli kiholea katika wakati huu wa kuelekea mwisho wa mwaka.

Katika hatua nyingine kiongozi huyo wa CHAKUA aliwataka abiria kuepuka vyakula au vinywaji wanavyopewa na watu wasiowafahamu wanapokuwa safarini kutokana na kuibuka kwa matukio ya wizi kwa njia mbalimbali zikiwamo za kuweka dawa za kulevya kwenye vinywaji au kwenye chakula.

“Tumepata taarifa ya watu kuibiwa kwa njia ya kupewa chakula au   vinywaji  vyenye dawa zinazosababisha usingizi  hivyo tunawaambia abiria wasipokee chakula au zawadi au kitu chochote kutoka kwa mtu wasiyemjua kwani wengine wanania mbaya,”aliongeza Mchanjama

Aidha aliongeza kuwa ni vyema abiria wakawa wakali kwa kutoa taarifa wanapobaini dereva anaendesha basi kinyume na utaratibu ikiwemo kwenda mwendo wa kasi au kuongea na simu wakati anaendesha gari ili kuweza kuepukana na ajali za mara kwa mara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,183FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles