Na MWANDISHI WETU – dar es salaam
KITENDO cha Rais Dk. John Magufuli kuitaka Wizara ya Kilimo ijitathmini kutokana na suala la mauzo ya korosho, kinatoa tafsiri kwamba mwenendo wa utendaji wake haumfurahishi.
Tafsiri hiyo inajenga mazingira ya wazi kwamba hata Waziri wa Kilimo, Dk. Charles Tizeba, naye huenda amekalia kuti kavu kutokana na kasoro za kiutendaji zinazojitokeza ndani ya wizara hiyo.
Wakati hali hiyo ikijitokeza wizarani hapo, tayari Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Profesa Wakuru Magigi, ameng’olewa katika nafasi hiyo kuanzia juzi kwa sababu ya kukiuka utaratibu wa uuzaji wa zao hilo.
Uamuzi wa kung’olewa kwa Profesa Magigi ulitokana na agizo la Rais Magufuli alilolituma kupitia kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ambaye juzi alilitekeleza mkoani Lindi wakati wa kikao chake na wakuu wa mikoa inayolima korosho.
Kwa mujibu wa maelezo yake, Majaliwa alisema …
Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.