24.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 27, 2023

Contact us: [email protected]

Mfanyabiashara adakwa na dawa za kulevya chooni

Na AGATHA CHARLES, DAR ES SALAAM


JESHI la Polisi kupitia Kikosi cha Operesheni Maalumu kilichopo chini ya Naibu Kamishna wa Polisi, Liberatus Sabas, limemkamata mfanyabiashara Kageta Kageta (35) akiwa na dawa za kulevya aina ya heroine zenye uzito wa gramu 815.3.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Sabas alisema tukio hilo lilitokea eneo la Tabata Kinyerezi, Dar es Salaam na mtuhumiwa alikutwa akiwa ameficha dawa hizo katika kontena chooni.

“Vyombo vya ulinzi na usalama vilipata taarifa na baada ya ufuatiliaji vilimtia mbaroni.

“Baada ya kumkamata na kumpekua alikutwa na dawa za kulevya aina ya heroine zenye uzito wa gramu 815.3.

“Dawa hizo zilikuwa zimefichwa eneo la chooni na kuwekwa kwenye kontena. Alipohojiwa amekiri kuwa alikuwa anajihusisha na biashara hiyo kwa muda mrefu,” alisema.

Sabas alisema wanatarajia kumfikisha mtuhumiwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

Alisema hawataruhusu kizazi cha Tanzania kupotea kutokana na dawa za kulevya na wataendelea kuwasaka watu wanaojihusisha na biashara hiyo popote walipo.

“Mtuhumiwa kama mnavyomuona ni mnene, anajinufaisha kwa biashara hiyo haramu ambayo inateketeza kizazi chetu cha kitanzania kwa sababu ya yeye kujitafutia kipato kisicho halali.

“Sisi tunasema hatutawaruhusu watu kama hawa wanaojijengea vitambi kwa kuwatafuta sehemu yoyote walipo na sheria itachukua mkondo wake,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,213FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles