27.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 20, 2023

Contact us: [email protected]

Marais Kenyatta, Akufo-Addo watoa somo kwa vijana Afrika

             Na MWANDISHI WETU, Lagos, Nigeria

MARAIS Uhuru Kenyatta wa Kenya na Nana Akufo-Addo wa Ghana wamewataka vijana Bara la Afrika kuwa wabunifu na kumchangamkia fursa za kiuchumi ili kuiweza kusaidia nchini zao.

Kauli hizo wametoa hivi karibuni jijini Lagos nchini Nigeria kwenye jukwaa la nne la kila mwaka lililoandaliwa na Taasisi ya Tony maarufu Tony Elumelu Foundation (TEF), Entrepeneurship Forum.

Rais Uhuru Kenyatta, aliwahimiza vijana kutoka bara la Afrika kutumia ubunifu wao ili kuleta mabadiliko.

“Viongozi vijana wabunifu kutoka Afrika wanapigana na mabadiliko yenye nia njema kwa kutumia teknolojia. Kuwa bora iwezekanavyo kwa familia, jamii, taifa yako lakini muhimu wewe mwenyewe,” amesema

Rais Uhuru alisisitiza ushauri wake kwa vijana kufanya kazi ili kuwa bora kwa taaluma ambayo wamechagua.

Tukio hilo ni fursa pekee ya kukusanya vipaji vya biashara kwa vijana, kujenga mitandao yenye nguvu na kupeleka ujumbe kwa watunga sera kwamba sekta binafsi iliyo mahiri na inawajibika inauwezo wa kuleta mabadiliko ya kiuchumi.

Baada ya kupata mafunzo ya miezi tisa, ushauri na ufadhili, jumla ya vijana 4,470 walifaidika na programu hiyo iliyoshuhudia zaidi ya vijana laki tatu wakituma maombi.

Mwasisi wa jukwaa hilo, Tony Elumelu, alisisitiza kuendelea kujitolea kuhakikisha maendeleo ya uchumi Afrika kwa kusaidia mafunzo ya kizazi kipya cha wajasiriamali ambao mafanikio yao yanaweza yakabadili bara hili ikwemo kutengeneza ajira.

“Ujasiriamali ni muhimu kufungua maendeleo ya uchumi katika bara letu. Naamini kwa dhati mafanikio yanaweza yakaleta demokrasia na kama tunaweza kubadili tamaa na kuwa fursa, hiki kizazi cha ajabu kinaweza kufanikiwa kwa kila jambo,” alisema Tony Elumelu

Naye Rais wa Ghana, Nana Akudo-Addo, aliwasisitizia wawakilishi wa sekta ya umma kuhimiza, kusaidia na kuiga kazi inayofanywa na Taasisi ya Tony Elumelu.

“Hakuna kinachobadilika au kujiendeleza kivyake. Watu lazima waamke, waonge, wajadili na kubadilisha mada,” alisema Rais Nana Akufo-Addo.

Tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo, imeweza kuwasaidia wajasiriamali Waafrika kutoka pembe zote za Bara la Afrika na washindi katika mashindano mbalimbali katika jukwaa la mwaka huu walipata ufadhili wa dola za Marekani 5000 (takribani Shilingi milioni 11.4 kila mmoja).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles