MOSCOW, Urusi
SERIKALI ya Urusi imesema imeishutukia Marekani kuamua kujitoa katika Mpango wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mkataba wa Nyuklia ( INF) kwa kile inachodai kuwa unaonekana ungeibana Washington katika mipango yake ya utawala wa jumla katika sekta ya kijeshi.
Taarifa hiyo imetolewa jana mjini hapa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Sergey Ryabkov, katika mahojiano na Shirika la Habari la nchi hii (TASS) kuhusu maoni yake juu ya taarifa ya Rais wa Marekani, Donald Trump kutangaza kujitoa katika mkataba wa kudhibiti silaha za nyukilia wa mwaka 1987.
Katika mahojiano hayo ya jana na TASS, Ryabkov alisema kuwa kwa mtazamo wake anaweza kusema inavyoonekana mkataba huo wa INF unasababisha vikwazo kwa Marekani kufuatia kuwa unainyima nchi hiyo utawala wa jumla katika nyanja ya kijeshi.
“Kwanza kwa mtazamo wangu naweza kusema kwamba inavyoonekana Mkataba wa INF unasababishwa vikwazo kwa Marekani kuelekea utawala wake katika nyanja za kijeshi.
“Inaonekana, kutokuwa na uwezo na hamu ya kujadiliana na sisi juu ya msingi wa sauti kushinikiza vikosi fulani huko Washington kuhamasisha uongozi wa nchi kufanya uamuzi juu ya kuondolewa rasmi kutoka mkataba huo,” alisema.
“Hii itakuwa hatua ya hatari sana, ambayo nina uhakika, haitaeleweka kwa jumuiya ya kimataifa na inaweza kuibua hasira za wanachama wote wa jamii hii ya kimataifa ambao wamejiunga na usalama na utulivu na wapo tayari kufanya kazi ya kuimarisha utawala wa sasa katika udhibiti wa silaha, “aliongeza Ryabkov.
Naibu waziri huyo alisema inaonekana wazi mkataba huo unainyima Marekani nafasi ya kujadiliana nao kuhusu kutuma vikosi fulani Washington ili kuhamasisha uongozi wa nchi kufanya uamuzi juu ya kuondolewa rasmi katika mkataba huo.
Alisema sababu hiyo ndiyo kubwa ambayo inaifanya Marekani kuamua kutangaza kujitoa katika mkataba huo ambao unajieleza moja kwa moja.
Hata hivyo Ryabkov aliiambia TASS kwamba wanatarajia ujio wa mshauri wa Marekani kuhusu masuala ya usalama katika Baraza la Umoja wa Mataifa, John Bolton aliyetarajiwa kuwasili mjini hapa jana ndiye atakayetoa ufafanunzi zaidi kuhusu uamuzi huo wa Washington kujitoa katika mkataba huo wa INF.
“Leo (jana) Mshauri wa Rais wa Marekani katika masuala ya usalama anawasili mjini hapa. Tuna matumaini wakati wa majadiliano naye kesho (leo) na kesho kutwa tutapata maelezo zaidi kuhusu hatua ambazo nchi hiyo inataka kuzichukua,”alisema Ryabkov.
Taarifa hiyo mekuja baada ya juzi Rais Trump, akizungumza na waandishi wa habari kusema kwamba Urusi ilikiuka mkataba huo wa wa mwaka 1987 unaofahamika kama Intermediate-Range Nuclear Forces (INF)
Mkataba huo ulipiga marufuku makombora yanayorushwa kutoka ardhini ambayo yanaweza kusafiri umbali wa kati ya kilomita 500 na 5,500.