27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Urusi yaishutukia Marekani kujitoa mpango wa nyuklia

MOSCOW, Urusi

SERIKALI ya Urusi imesema imeishutukia Marekani kuamua kujitoa katika Mpango  wa  Umoja wa Mataifa  kuhusu Mkataba wa Nyuklia ( INF) kwa kile inachodai kuwa unaonekana ungeibana Washington katika mipango yake ya  utawala wa jumla katika sekta ya kijeshi.

Taarifa hiyo imetolewa jana mjini hapa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Sergey Ryabkov, katika mahojiano na Shirika la Habari la nchi hii (TASS) kuhusu  maoni yake  juu ya taarifa ya Rais wa Marekani, Donald Trump  kutangaza kujitoa katika  mkataba wa kudhibiti silaha za nyukilia wa mwaka  1987.

Katika mahojiano hayo ya jana na TASS, Ryabkov alisema kuwa kwa mtazamo wake anaweza kusema inavyoonekana mkataba huo wa INF unasababisha vikwazo  kwa Marekani kufuatia kuwa unainyima nchi hiyo utawala wa jumla katika nyanja ya kijeshi.

“Kwanza kwa mtazamo wangu  naweza kusema kwamba inavyoonekana  Mkataba wa INF unasababishwa vikwazo kwa Marekani  kuelekea utawala wake  katika nyanja za kijeshi.

“Inaonekana, kutokuwa na uwezo  na hamu ya kujadiliana na sisi juu ya msingi wa sauti kushinikiza vikosi fulani huko Washington kuhamasisha uongozi wa nchi kufanya uamuzi juu ya kuondolewa rasmi kutoka mkataba huo,” alisema.

“Hii itakuwa hatua ya hatari sana, ambayo  nina uhakika, haitaeleweka kwa  jumuiya ya kimataifa na inaweza kuibua hasira za  wanachama wote wa jamii hii ya kimataifa  ambao wamejiunga na usalama na utulivu na wapo tayari kufanya kazi ya  kuimarisha utawala wa sasa katika udhibiti wa silaha, “aliongeza Ryabkov.

Naibu waziri huyo alisema inaonekana wazi mkataba huo unainyima Marekani nafasi ya kujadiliana nao kuhusu kutuma  vikosi fulani  Washington  ili kuhamasisha uongozi wa nchi kufanya uamuzi juu ya kuondolewa rasmi katika  mkataba huo.

Alisema sababu hiyo ndiyo kubwa ambayo inaifanya Marekani kuamua kutangaza kujitoa katika mkataba huo ambao unajieleza moja kwa moja.

Hata hivyo Ryabkov aliiambia TASS kwamba wanatarajia ujio wa mshauri wa Marekani kuhusu masuala ya usalama katika Baraza la Umoja wa Mataifa,  John Bolton aliyetarajiwa kuwasili mjini hapa jana ndiye atakayetoa ufafanunzi zaidi kuhusu uamuzi  huo wa Washington kujitoa katika mkataba huo wa INF.

“Leo (jana) Mshauri wa Rais wa Marekani katika masuala ya usalama anawasili mjini  hapa. Tuna matumaini wakati wa majadiliano naye kesho (leo) na kesho kutwa tutapata maelezo zaidi  kuhusu hatua ambazo nchi hiyo inataka kuzichukua,”alisema  Ryabkov.

Taarifa hiyo mekuja baada ya juzi Rais  Trump, akizungumza na  waandishi wa habari kusema kwamba Urusi ilikiuka mkataba huo wa wa mwaka 1987 unaofahamika kama Intermediate-Range Nuclear Forces (INF)

Mkataba huo ulipiga marufuku makombora yanayorushwa kutoka ardhini ambayo yanaweza kusafiri umbali wa kati ya kilomita 500 na 5,500.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles