32.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 1, 2023

Contact us: [email protected]

Watu 55 wafa katika mapigano  sokoni Nigeria

LAGOS,Nigeria

RAIS  Muhammadu Buhari amesema watu wapatao  55  wamepoteza maisha kufutia ghasia zilizozuka katika soko moja lililopo katika Jimbo la Kaduna,  Kaskazini mwa Nigeria.

Vifo hivyo vinaripotiwa kutokea baada ya  vijana wa Kikristo na Kiislamu  wasukuma mikokoteni kuanza kupigana  katika soko hilo lililopo katika mji wa  Kasuwan Magani.

Kamishna wa Polisi wa Jimbo hilo, alisema kwamba watu zaidi ya  22  wanashikiliwa na jeshi lake na kwamba wameshatangaza hali ya hatari katika mji huo kufuatia machafuko hayo.

“Bila kuwapo uwelewano kati ya makundi tofauti, biashara zetu haziwezi kuendelea,” alisema Rais Buhari.

Alitoa wito kwa viongozi wa jumuiya kuhimiza uvumilivu na kuacha ugomvi huo kabla ya kuendelea na kuwa vurugu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles