26.6 C
Dar es Salaam
Saturday, November 30, 2024

Contact us: [email protected]

Anayedai kufanyiwa ukatili kijinsia na Rais Trump akubali kutoa ushahidi

NEW YORK, Marekani

Mwanamke   ambaye amefungua madai ya unyanyasaji wa kijinsia  na kutishia kumfikisha mahakamani Rais wa Marekani, Donald Trump,  amekubali kutoa ushahidi wake baadae wiki hii.

Uamuzi huo wa Christine Blasey Ford umekuja, baada ya kujadiliana na wanasheria wake kwa siku kadhaa, huku  Rais  Trump akisema tuhuma hizo haziwezi kuwa na ukweli wowote.

Hata hivyo juzi baada ya Kamti ya Maseneta kupokea ujumbe kutoka kwa mawakili wa  Ford wajumbe kadhaa wa kamati hiyo walikubali kupokea ushahidi wake.

“Dkt. Blasey Ford atatoa ushuhuda wake wiki ijayo. Ameonyesha ujasiri mkubwa katika kukabiliwa na vitisho vya kifo na unyanyasaji na anastahili heshima kama maelezo ya mwisho ya kusikilizwa yanafanyika, “Seneta wa  wa Chama cha Democratic,  Dianne Feinstein aliandika kupitia  ukurasa wake wa Twitter.

Muda mfupi baada ya kutumwa ujumbe huo na nyingine  kutoka kwa maseneta wengine zilifuatia  wakikariri chanzo cha  habari kutoka ndani ya familia kilieleza kuwa mwanamke huyo atatoa ushahidi wake Alhamisi wiki hii.

Kiongozi wa kamati hiyo, Chuck Grassley alisema walitaka mwanamke huyo atoe ushahdi huo Jumatano wiki hii lakini mwenyewe akaomba iwe mapema Alhamisi  ili aweze kumleta mtu ambaye anadai alikuwapo wakati  wa shambulizi hilo.

Akizungumza kuhusu tuhuma hizo, Rais  Trump, alisema kwamba kutokana na ukimya wa muda mrefu aliokuwa nao mwanamke huyo ina maana kwamba jambo hilo halikumtokea.

“Sina wasiwasi katika hilo kama ningefanya shambulizi dhidi ya Dk Ford lingekuwa baya angekuwa alishasema,”alisema Rais Trump.

 

Mwisho

 

Rais Putin atuma salamu za rambirambi

Iran

 

MOSCOW,  Urusi

 

RAIS Vladimir Putin wa Urusi, ametuma salamu za rambi rambi kwa mwezake wa Iran, Hassan Rouhani kutokana na vifo vya wanajeshi waliopoteza maisha katika shambulizi la kigaidi katika mji wa  Ahvaz.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana mjini hapa  kupitia tovuti ya Ikulu, Rais Putin alielezea kusikitishwa sana na shambulizi hilo na akasema kwamba hawataweza kuvumilia kuona matukio hayo yakizidi kuongezeka.

 

“Mpendwa mheshimiwa Rais, tafadhali pokea salamu zetu za majonzi  kutokana na matukio mabaya ya uvamizi wa kigaidi katika Jiji la Ahvaz. Tukio hili mara nyingine tena linatukumbusha juu ya kuungana katika vita  dhidi ya ugaidi.

Ninathibitisha nitashirikiana na nchi yako kukabiliana na uovu huu,”alisema Rais Putin kupitia taarifa aliyoituma kwa njia ya telegram.

Mbali na kumtumia Rais mwenzake salamu hizo Rais Putin pia aliwatumia ndugu na marafiki ambao waliuawa huku akiwatakia kupona kwa haraka wote waliojeruhiwa.

 

Tukio hilo ambalo lilitokea juzi, baada ya wanaume waliokuwa wamevaa sare za kijeshi kushambulia gwaride hilo la  jeshi linadaiwa kusababisha vifo vya wanajeshi  24 na kujeruhi wengine  53.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles