Rais Putin atuma salamu za rambirambi

0
1340

MOSCOW,  Urusi

Rais  Vladimir Putin wa Urusi, ametuma salamu za rambi rambi kwa mwezake wa Iran, Hassan Rouhani kutokana na vifo vya wanajeshi waliopoteza maisha katika shambulizi la kigaidi katika mji wa  Ahvaz.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana mjini hapa  kupitia tovuti ya Ikulu, Rais Putin alielezea kusikitishwa sana na shambulizi hilo na akasema kwamba hawataweza kuvumilia kuona matukio hayo yakizidi kuongezeka.

“Mpendwa mheshimiwa Rais, tafadhali pokea salamu zetu za majonzi  kutokana na matukio mabaya ya uvamizi wa kigaidi katika Jiji la Ahvaz. Tukio hili mara nyingine tena linatukumbusha juu ya kuungana katika vita  dhidi ya ugaidi.

Ninathibitisha nitashirikiana na nchi yako kukabiliana na uovu huu,”alisema Rais Putin kupitia taarifa aliyoituma kwa njia ya telegram.

Mbali na kumtumia Rais mwenzake salamu hizo Rais Putin pia aliwatumia ndugu na marafiki ambao waliuawa huku akiwatakia kupona kwa haraka wote waliojeruhiwa.

Tukio hilo ambalo lilitokea juzi, baada ya wanaume waliokuwa wamevaa sare za kijeshi kushambulia gwaride hilo la  jeshi linadaiwa kusababisha vifo vya wanajeshi  24 na kujeruhi wengine  53.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here