32.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 22, 2024

Contact us: [email protected]

WANAKIJIJI ARUMERU WAFURAHIA KUPATA MAWASILIANO

Na MWANDISHI WETU  – ARUSHA


WAKAZI wa Kijiji cha Timbolo, Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, wamepongeza jitihada za mtandao wa simu wa Halotel kwa kufikisha mawasiliano kijijini hapo baada ya kuhangaika kwa muda mrefu kupata huduma za mawasiliano ya uhakika, jambo ambalo limechangia kwa ukuaji wa shughuli za kiuchumi kwa wakazi wa kijiji hicho, hususani huduma jumuishi za fedha.

Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Samwel Kivuyo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali walipokwenda kutembelea katika kijiji hicho ili kuona na kujifunza shughuli mbalimbali za kimaendeleo ambazo zimechangiwa na mtandao huo kuwekeza katika maeneo ambayo awali hayakuwa na huduma za mawasiliano ya uhakika.

“Halotel wamesaidia sana kufikisha huduma jumuishi za kifedha kwa wananchi masikini wa kijiji hiki ambao awali walikuwa wanataabika na kupitwa na huduma hizo, hivyo kulazimika kutembea kilomita nyingi kufuata huduma za kifedha, kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kijiji hicho.

“Mpaka sasa hali ya mawasiliano katika kijiji chetu ni nzuri, watu wamepata ajira kufuatia kuanzisha biashara za huduma za kifedha kwa njia ya simu pamoja na kuongeza uzalishaji wa mazao ya mbogamboga ambayo ni kazi kuu ya wanakijiji wetu, kwani mara ya kwanza mawasiliano na wafanyabiashara wengine yalikuwa ni magumu, ila sasa tuna uhakika wa wateja kwa sababu tunawasiliana nao,” alisema Kivuyo.

Mwenyekiti huyo alibainisha kuwa hadi sasa changamoto inayowakabili kijijini hapo ni ukosefu wa umeme katika kijii hicho, jambo ambalo linatatiza shughuli za maendeleo kwa baadhi ya wananchi.

Baadhi ya wanakijiji katika Kata ya Sambasha wameelezea kufurahishwa na huduma ya Halopesa, wamesema imekuwa rafiki kulinganisha na huduma kama hizo zinazotolewa na kampuni nyingine kutokana na Halotel kutotoza makato pindi mtumiaji wa huduma hiyo akituma pesa kwenda mtandao huo.

“Kwakweli ukiwa na huduma za Haloteli unafurahia kupata muda wa maongezi wa kutosha, data ndiyo siwezi kuelezea, yaani ni huduma rafiki sana kwa sisi, hasa wa huku kijijini ambao kipato chetu ni cha chini,” alisema Rehema Joshua, mkazi Kijiji cha Timbolo.

Alipotafutwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro, kutaka kufahamu namna Serikali inavyoweza kuwasaidia wananchi hao, alisema tayari zimeshafanywa jitihada za kufungiwa mfumo wa umeme majumbani mwao.

“Kwakweli nawapongeza wananchi hao wa Kijiji cha Timbolo kwa jitihada zao na Serikali inafurahishwa mno na aina ya wanachi wanaopenda kujiletea wenyewe maendeleo.

“Na nimemtaka Mwenyekiti wa Kijiji cha Timbolo, Samwel Kivuyo, aje wakati wowote ofisini kwangu akiwa na wawakilishi watatu wa wanakijiji tuzungumze na kumaliza mara moja kadhia hiyo ya umeme,” alisema DC Muro.

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Mawasiliano, Kampuni ya Halotel Tanzania, Mhina Simwenda, alisema kuwa Halotel Tanzania ipo mkoani Arusha kwa ajili ya kuongea na wateja, kusikiliza maoni kutoka kwao, kujua wanahitaji nini, kujua changamoto walizonazo ili waweze kuboresha huduma zao kwa wateja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles