25.5 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

DIWANI APANDISHWA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA WIZI

Na SEIF TAKAZA – IRAMBA


JESHI la Polisi wilayani Iramba, Mkoa wa Singida, limewafikisha mahakamani watu 19 wakazi wa Kijiji cha Nguvumali, kwa tuhuma ya kuiba vifaa vya ujenzi wa Kituo cha Afya Ndago.

Miongoni mwa waliofikishwa katika Mahakama hiyo ya Wilaya ya Iramba juzi ni Diwani wa Kata ya Ndago, Henry Nkhandi na Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho, Yasin Nyawangele.

Mwendesha Mashtaka wa Mahakama, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Salumu Nannume, aliiambia mahakama hiyo mbele ya Hakimu Makwaya Charles, kwamba washtakiwa hao walitenda kosa hilo Agosti 3, mwaka huu baada ya kuvunja stoo ya vifaa vya ujenzi na kuiba vifaa hivyo.

Mwendesha Mashtaka Nannume aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Emmanuel Shalua (40), Diwani Nkhandi, Anton Mkumbo (43), Geofrey Selemani (43), Joseph Kitila (50), Shamir Ramadhani (23), Amos Nkana (45) na Rachel John (46).

Wengine ni Jackline Shabani (35), Grace Lyanga (56), Uswili Jackson (54), Elisha Tertlano (52), Maria Yohana (34), Kidyson Kidindima (49), Hawa Swahehe (35), Babu Musa (22), Catherine Songelaeli(35), Emanuel Manase (23) na Yasini Nyawengele ambaye ni Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Ndago.

Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka huyo, watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Agosti 3, mwaka huu, majira ya usiku ambapo walivunja stoo na kuiba vifaa vya ujenzi wa Kituo hicho cha Afya Ndago vyenye thamani ya Sh milioni 9.8.

Alivitaja baadhi ya vifaa hivyo kuwa ni saruji, nondo, vigae, mbao na vifaa vingine.

Washtakiwa hao walikana mashtaka na wako nje kwa dhamana hadi Septemba 10, mwaka huu, kesi yao itakapotajwa tena.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles