TANESCO YAZALISHA UMEME WA KUTOSHA

0
1388

Na MWANDISHI WETU – DODOMA


SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco), limesema  linazalisha umeme wa kutosha mahitaji ya nchi, huku ziada ikiwa ni zaidi ya megawati 200 na hivyo kupelekea kupungua kwa changamoto ya kukatika umeme mara kwa mara.

Hayo yamesemwa jana jijini Dodoma na Mkurugenzi  Mtendaji wa Tanesco,  Dk. Tito Mwinuka, wakati akiwasilisha taarifa ya shirika hilo kwa Kamati  ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.

Alisema umeme unaozalishwa sasa ni takribani megawati 1517.47, huku matumizi yakiwa ni takribani ni megawati 900.

Dk. Mwinuka alisema shirika hilo linaendelea na juhudi za kuwaunganishia umeme wananchi, kazi ambayo inakwenda  sambamba na kuimarisha mifumo ya usafirishaji na usambazaji wa umeme ili kupunguza matukio ya kukatika kwa umeme mara kwa mara.

Kutokana na jitihada hizo, mapato ya Shirika yamekuwa yakiongezeka mwaka hadi mwaka na kuliwezesha Shirika kujiendesha bila kutegemea ruzuku kutoka serikalini tangu mwaka 2015/16.

“Mapato ya Shirika yameendelea kuimarika, ambapo katika kipindi cha mwaka 2017/18, makusanyo yamekuwa ya wastani wa shilingi bilioni 38 hadi 39 kwa wiki kutoka wastani wa shilingi bilioni 34 katika mwezi Aprili, 2018,” alisema Dk. Mwinuka.

Akizungumzia suala la deni la Tanesco, Dk. Mwinuka, alisema kuna sababu mbalimbali zinazopelekea deni la Shirika kuongezeka, ikiwa ni pamoja na gharama kubwa za uzalishaji wa umeme katika maeneo yaliyopo mbali na gridi ya Taifa ambapo Tanesco hulazimika kuzalisha umeme kwa wastani wa Sh 763 kwa uniti moja.

Alieleza juhudi mbalimbali zinazofanywa na Tanesco ili kupunguza madeni kwa shirika ni kutafuta mikopo yenye masharti nafuu, kuongeza mapato na kupunguza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here