33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

WATU 700 WA VIRUSI VYA UKIMWI WATOWEKA

Na SEIF TAKAZA, SINGIDA                  |                          


ZAIDI ya waathirika wa ugonjwa wa  Ukimwi 700 katika Halmashauri ya  Wilaya ya Mkalama Mkoa wa Singida, waliokuwa wakitumia  dawa za ARVs kwa ajili  kufubaza ugonjwa huo hawajulikani walipo.

Hayo yalisemwa juzi katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika mjini Nduguti.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudhibiti Ukimwi katika Halmashauri hiyo ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Dia Kambi alisema hali hiyo ni mbaya na hatua za haraka zinapaswa kuchukuliwa.

‘’Waheshimiwa madiwani, nasikitika kuwaeleza kuwa waathirika 703 wa Ukimwi waliokuwa wakitumia dawa za ARV hawajulikani walipo.

“Kamati yangu na uongozi wa halmashauri inabidi kufanya jitihada za kuwatafuta kwa juhudi zote  warudi kupata dawa hizi…ni hatari wanaweza kupoteza maisha kwa mujibu wa wataalamu wa afya,’’ alisema Kambi.

Alisema changamoto kubwa inayokabili huduma hiyo ni pamoja na waathirika kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu madhara ya kuacha kutumia dawa hizo.

Naye Diwani wa Kata ya Kinyangiri, Asma Seif alisema hali hiyo  inatokana na huduma kuwa mbali na huduma ya kutolea dawa.

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles