32.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

WATUMIAJI WA KEMIKALI WAONYWA

 

 

Na AZIZA MASOUD,DAR ES SALAAM


SERIKALI imewataka watumiaji wa kemikali nchini kuzitumia kwa usahihi na kufuata sheria za matumizi ya bidhaa hiyo, ili kuepuka madhara yanayosababishwa na utumiaji usiofuata taratibu.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkurugenzi Msaidizi Mazingira, Ofisi ya Makamu ya Rais, Magdalena Mtenga, wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku mbili ya wadau wanaojishughulisha na  masuala ya kemikali kupitia kemikali taka iliyoandaliwa na Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA).

Alisema matumizi ya kemikali hayaepukiki kutokana na maendeleo ya teknolojia na kwamba kemikali inatumika pia majumbani hivyo zinapaswa kutumiwa kwa uangalifu ili kuepuka madhara.

“Iko haja ya kuwa na matumizi sahihi ya kemikali kwani kutoitumia katika matumizi sahihi husababisha athari mbalimbali, wapo watu wanaopata ulemavu kwa kemikali wanapozitumia vibaya,” alisema Mtenga.

Alisema Serikali imechukua hatua mbalimbali kuhakikisha kemikali zinatumika katika matumizi sahihi na salama kwa kufuata sheria, kanuni, sera na miongozo iliyopo.

Alisema pia Serikali imechukua hatua mbalimbali za kuzuia athari za kemikali ambapo pia kupitia warsha hiyo washiriki watajadili mikataba mbalimbali ikiwemo ya usafirishaji wa kemikali taka kutoka nchi moja kwenda nyingine.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi Mkemia Mkuu wa Serikali, Dk. Fidelice Mafumiko, alisema warsha hiyo  inayowakutanisha watu wanaoshughulikia kemikali na kemikali taka, inalenga kuwajengea uwezo wadau hao ambao wanaamini watatoa maoni kuhusu namna nzuri ya kutumia kemikali hizo.

Alisema washiriki watapata fursa ya kusikiliza mada zitakazotolewa na wataalamu waliobobea katika masuala ya kemikali na kemikali taka na kwamba mwisho wa warsha washiriki watakuwa na uelewa mpana.

Alisema udhibiti wa kemikali na kemikali taka ni kwa lengo la kulinda afya za wananchi na uchafuzi wa mazingira.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles