20.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 28, 2022

MADA MAUGO ATAMBA KUMCHAKAZA MISANJO

NA LULU RINGO


BONDIA ngumi za kulipwa nchini, Mada Maugo, ametamba  kumchapa mpinzani wake Charles Misanjo kutoka Malawi  kwa K.O,  katika pambano litakalofanyika kesho kwenye Ukumbi wa PTA, Sabasaba, Dar es Salaam.

Pambano hilo la raundi 12, ni kwa ajili ya la kuchangia taulo za kike kwa wanafunzi wa shule za sekondari za mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ambapo lengo ni kupata taulo 40,000.

Akizungumza leo wakati wa kupima uzito, katika viwanja vya Las Vegas, jijini Dar es Salaam, Maugo, alisema amejiandaa  kumaliza pambano hilo mapema kwa kumpiga mpinzani wake kwa K.O.

Maugo aliwataka mashabiki wa mchezo wa ngumi kufika kwa wingi ili kufanikisha mchakato huo wa kusaidia wasichana kupata taulo hizi wanazotumia wakiwa katika siku za hedhi.

“Misanjo sio bondia wakunitisha mimi, nishakutana na mabondia wengi nchi tofauti na nimewapiga, naomba tu mashabiki wajitokeze kuona wenyewe, pia  waweze kutoa mchango wao kuanikisha zoezi hili,” alisema Maugo.

Tofauti na Maugo, mabondia wengine watakaopanda ulingoni ni Ibrahim Class dhidi ya Maina Mazora na litakuwa la raundi nane.

Wengine ni wanawake, Asha Ngedere dhidi Happy Daudi na Frola Machele atazipiga na  Sarafina  Julius, mapambano yote yatakuwa ya raundi sita.

Kwa upande wake Mratibu wa mapambano hayo, Mbunge wa viti Maalum Mbeya, Sophia Mwakagenda, alisema  wanahitaji sapoti ya Watanzania, kufanikisha mchakato huo.

Alisema njia pekee ya kuchangia ni kufika ukumbini siku ya mchezo huo kwa sababu viingilio vyao ndio vitatumika  kununulia taulo hizo.

“Hata kwa wale ambao hawatafika, wanaweza kuchangia, tunapokea hata boksi moja la taulo hizo, lengo zifike 40,000, ikiwezekana ziwe zaidi kwa sababu mahitaji ni makubwa,” amesema Mwakagenda.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,097FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles