MOSCOW, URUSI
KUNA baadhi ya timu zilipewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Urusi, hii ni kutokana na ubora wa vikosi vyao pamoja na historia.
Miongoni mwa timu hizo ni pamoja na Hispania, Ujerumani, Ureno, Ufaransa na  Argentina, lakini  kinyume na matarajio ya mashabiki wengi wa soka zimeshindwa kuthibitisha hilo baada ya kujikuta zikifungashiwa virago mapema.
Ujerumani
Timu hiyo iliingia kwenye michuano hiyo huku ikiwa ni mabingwa watetezi kutokana na kutwaa taji hilo mwaka 2014 nchini Brazil ilipomfunga mpinzani wake Argentina bao 1-0.
Wengi waliamini Ujerumani ingefanya vizuri nchini Urusi kwa kutwaa ubingwa au kufika mbali kama vile hatua ya robo fainali, nusu na fainali, lakini haikuwa hivyo badala yake ilifungashiwa virago katika hatua ya makundi.
Ujerumani ilikuwa na baadhi ya mastaa ambao wanafanya vizuri kwenye ligi mbalimbali Ulaya, lakini mifumo ya kocha wao, Joachim Low, haikwenda sawa na wachezaji hao hatimaye kujikuta wakiwa kwenye wakati mgumu na kushindwa kufanya vizuri.
Hispania
Ukizungumzia klabu zenye wachezaji bora duniani kwa sasa huwezi kuziweka kando Real Madrid na Barcelona.
Klabu hizi mbili pinzani ndizo zilizochangia idadi kubwa ya wachezaji waliounda kikosi cha timu ya taifa ya Hispania.
Barcelona ilifanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu na Copa del Ray huku Real Madrid ikitwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliomalizika hivi karibuni, lakini………
Kupata habari kamili jipatie nakala ya gazeti lako la MTANZANIA hapo juu