32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

UTAFITI: JOTO HUCHANGIA WATU KUSHINDWA MITIHANI

LOS ANGELES, MAREKANI


UTAFITI uliofanywa na watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Harvard na vyuo vingine vikuu vya Marekani, umebainisha uwapo wa uhusiano kati ya viwango vya juu vya joto na mafanikio shuleni.

Vipimo vya uchanganuzi wa alama kwa wanafunzi 10 wa shule za sekondari, vilivyochukuliwa kwa kipindi cha miaka 13 ya joto, vinaonyesha majira ya joto yana athari hasi kwa matokeo shuleni.

Utafiti huo unasema labda njia ya kukabiliana na athari hiyo inaweza kuwa ni kutumia viyoyozi zaidi.

Wanafunzi wanaofanya mitihani wakati wa majira ya joto, wamekuwa wakilalamika kuwa wanasumbuliwa na joto.

Lakini utafiti huu kutoka kwa wasomi wa vyuo vikuu vya Havard, California (UCLA) na kile cha taifa cha Georgia, wanadai kupata ushahidi unaonyesha uhusiano wa joto na matokeo ya mitihani ya kushuka.

Utafiti huo uliochapishwa na Taasisi ya Uchunguzi wa Kiuchumi Marekani, ulibaini wanafunzi walikuwa na uwezekano mkubwa wa kuwa na alama za chini wakati wa majira ya joto na matokeo mazuri wakati wa majira ya baridi.

Matokeo haya yalikuwa sawia kwenye maeneo yenye tabia nchi tofauti kama vile majimbo yenye baridi zaidi ya kaskazini mwa Marekani au yenye viwango vya joto ya kusini.

Utafiti huo kuhusu joto na masomo, unasema hali ya hewa ya joto huwafanya wanafunzi washindwe kujifunza na kuwa makini wanapofanya kazi wanazopewa shule wazifanyie nyumbani.

Umebaini pia kuwapo kwa athari za hali ya hewa ya joto katika uchumi wa familia zenye kipato cha chini na wanafunzi wanaotoka katika jamii za walio wachache.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles