30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 25, 2022

MAREKANI, TANZANIA KUPAMBANA NA VVU/UKIMWI

Na FERDINDA MBAMILA-DAR ES SALAAM


WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa na Kaimu Balozi wa Marekani hapa nchini, Inmi Patterson, wamezindua kampeni ya maadhimisho ya miaka 15 ya ubia kati ya Marekani na Tanzania katika kupambana na janga la VVU/Ukimwi, chini ya Mpango wa Rais wa Marekani wa Kupambana na Ukimwi (PEPFAR).

Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana, ambako  Kaimu Balozi alitangaza pia kuwa, hivi karibuni PEPFAR imevuka lengo muhimu katika utoaji huduma hapa nchini, ambako hivi sasa inatoa matibabu yanayookoa maisha kwa zaidi ya Watanzania milioni moja wanaoishi na VVU.

Alisema tangu kuzinduliwa kwa PEPFAR na Rais George W. Bush hapo mwaka 2003, Serikali ya Marekani imewekeza zaidi ya Dola za Kimarekani bilioni 4.5 (takriban Sh trilioni 10.26) katika kudhibiti maambukizi ya VVU/Ukimwi nchini.

“Kampeni mpya ya PEPFAR15 itaendelea kwa mwaka huu ili kuadhimisha mafanikio yaliyofikiwa na nchi zetu mbili katika mapambano dhidi ya VVU na kuendelea kuchukua hatua stahili za kudhibiti kuenea kwa VVU nchini Tanzania.

“Wakati wa kampeni hii, tutafanya kazi nanyi nyote, pamoja na watu wanaoishi na VVU nchini kote Tanzania, ili kusimulia hadithi na habari nzuri (positive stories); habari za watu wanaoishi na VVU ambao wakati mmoja walikuwa dhaifu na wagonjwa.

“Lakini sasa wakiwa wenye nguvu na afya, habari za watu waliopima mapema na kuanza matibabu hata kabla hawajaanza kuumwa, habari za watu wanaoishi na VVU walioanza matibabu ya kuokoa maisha ili pia kuwalinda wenza wao na habari za akina mama wanaoishi na VVU wanaopata matibabu ili kuwalinda watoto wao,” alisema Kaimu Balozi Inmi Patterson.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
201,896FollowersFollow
553,000SubscribersSubscribe

Latest Articles