HAVANA,Cuba
MAOFISA wa Serikali ya Cuba wamesema kuwa wamefanikiwa kupata kisanduku cheusi kimoja ambacho kilikuwa  kinarekodi mwenendo wa ndege ambayo ilianguka juzi karibu na Uwanja wa Ndege wa Havana na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 100  kikiwa katika hali nzuri.
Taarifa hiyo imetolewa jana na Waziri wa Usafrishaji, Â Adel Yzquierdo na akasema kwamba wana matumaini kisanduku kingine cha pili kitapatikana hivi karibuni.
Katika ajali hiyo maofisa hao walisema watu 110 wakiwamo raia wa kigeni 11 na walionusurika ni wanawake watatu ambao wanasemekana kuwa hali zao ni mbaya baada ya  kuungua vibaya.
Tukio linatakuwa  ni la kwanza baya kuikumba nchi hiyo katika kipindi cha muongo mmoja na  tayari siku mbili za maombolezo zilizotangazwa tangu siku hiyo ya ajali zimeshaanza.
Maofisa hao wa serikali walisema uchunguzi wa chanzo cha kuanguka  ndege hiyo aina ya  Boeing 737 ambayo imefanya kazi kwa muda wa miaka karibia  40 umeshaanza.