27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

PUTIN AAHIDI KUISAIDIA UINGEREZA UCHUNGUZI KACHERO ALIYEPEWA SUMU

SOCHI, Urusi


RAIS wa Urusi, Vladimir Putin  amesema kwamba nchi yake bado inaendelea na msimamo wake wa kuisaidia Uingereza katika kuchunguza tukio la kupewa sumu  kachero wake wa zamani, Sergei Skripa

Kwa mujibu wa Shirika la Habari nchini  hapa, TASS, Rais Putin aliyasema hayo mwishoni mwa wiki, baada ya kukutana  na Kansela wa Ujerumani,  Angela Merkel aliyekuwapo ziarani.

Alisema,  alivyoahidi tangu mwanzo   serikali yake ina dhamira ya dhati kuwa sehemu ya uchunguzi huo na kwamba licha ya kuwa bado hawajajibiwa, lakini wapo tayari kufanya hivyo.

“Narudia kusema tena sisi tunataka kusaidiana na Uingereza katika kuchunguza tukio hilo na licha ya kuwa bado hatujajibiwa , lakini ofa yetu ipo pale pale,”alisema Rais Putin.

Alisema, anajivunia sana  baada ya kusikia katika vyombo vya habari kuwa, Skripal ameruhusiwa kutoka hospitali alipokuwa amelazwa na akamtakia afya njema.

Kachero huyo wa jeshi mwenye umri wa miaka 66 ambaye aliwahi kuhukumiwa nchini hapa kwa tuhuma za kutumiwa na Uingereza   na bintiye,  Yulia, 33, Machi 4 mwaka huu walikutwa  wakiwa katika hali mbaya kwenye  benchi lililopo karibu na duka la  Maltings  mjini Salisbury.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles