30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 25, 2022

KISANDUKU CHA KWANZA NDEGE ILIYOANGUKA CHAPATIKA

HAVANA,Cuba


MAOFISA  wa Serikali ya Cuba wamesema kuwa wamefanikiwa kupata kisanduku cheusi  kimoja ambacho  kilikuwa  kinarekodi mwenendo wa ndege ambayo ilianguka juzi karibu na Uwanja wa Ndege wa Havana  na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 100  kikiwa katika hali nzuri.

Taarifa hiyo imetolewa jana na Waziri wa Usafrishaji,  Adel Yzquierdo na akasema kwamba wana matumaini kisanduku kingine cha pili kitapatikana hivi karibuni.

Katika ajali hiyo maofisa hao walisema watu 110 wakiwamo raia wa kigeni 11 na walionusurika ni wanawake watatu ambao wanasemekana kuwa hali zao ni mbaya baada ya  kuungua vibaya.

Tukio linatakuwa  ni la kwanza baya kuikumba nchi hiyo katika kipindi cha muongo mmoja na  tayari siku mbili za maombolezo zilizotangazwa tangu siku hiyo ya ajali zimeshaanza.

Maofisa hao wa serikali walisema uchunguzi wa chanzo cha  kuanguka  ndege hiyo aina ya  Boeing 737 ambayo imefanya kazi kwa muda wa miaka  karibia  40 umeshaanza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
201,896FollowersFollow
553,000SubscribersSubscribe

Latest Articles