Na MWANDISHI WETU-DODOMA
MWENYEKITI wa Bunge, Mussa Zungu, ameiagiza Kamati ya Bunge ya Bajeti, ikutane na wabunge wawili wa CCM, waliotishia kukwamisha bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa mwaka wa fedha 2018/19, iliyowasilishwa na Waziri wa Kilimo, Dk. Charles Tizeba.
Zungu alifikia hatua hiyo baada ya wabunge hao, Nape Nnauye wa Mtama na Hussein Bashe wa Nzega Mjini, kutishia kukwamisha bajeti hiyo baada ya kutoridhishwa na majibu ya Dk. Tizeba kuhusu sekta ya kilimo.
Pamoja uamuzi huo, Dk. Tizeba juzi alilazimika kuviondoa baadhi ya vifungu vilivyoibua utata wakati Bunge lilipoketi kama Kamati ya Matumizi.
Aliyekuwa wa kwanza kuonyesha nia hiyo, huku akisema atashika shilingi ya bajeti ya wizara hiyo, ni Nape ambaye pamoja na mambo mengine, alisema haridhishwi na hatua zilizochukuliwa na Serikali katika zao la korosho, akijielekeza katika fedha zinazotokana na ushuru wa mauzo ya nje ya nchi (export levy).
“Mheshimiwa mwenyekiti, asubuhi nilieleza jinsi wakulima wa nchi hii wakiwamo wale wa korosho walivyosahaulika.
“Sasa nasema hivi, kama majibu yanayotolewa na Serikali yataendelea kutoniridhisha, nitakamata shilingi ya mshahara wa waziri hadi vikwazo vya wakulima wa korosho kuhusu kuondolewa kwa export levy vitakapokuwa vimeondolewa,” alisema Nape.
Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.