23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

MAGUFULI ATOA MWEZI MMOJA WADAIWA JWTZ

ELIZABETH HOMBO na NORA DAMIAN-DAR ES SALAAM


RAIS Dk. John Magufuli, amezitaka taasisi za Serikali na binafsi kulipa deni la Sh bilioni 41.4 ndani ya mwezi mmoja, zinazodaiwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

Amesema ndani ya muda huo kama bado hazijalipa, vyombo vyote vya ulinzi na usalama vitatumia nguvu.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (JWTZ), Jenerali Venance Mabeyo, taasisi hizo zinadaiwa Sh bilioni 38 huku kampuni ya ulinzi ya SUMA ikidai Sh bilioni 3.4.

Kutokana na hilo, Rais Magufuli alimwagiza Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Ali Mwinyi, kuziandikia barua taasisi hizo zinazodaiwa huku akimtaka nakala nyingine amkabidhi ili na yeye afuatilie deni hilo.

Mkuu huyo wa nchi alitoa kauli hiyo jana alipozindua Kituo cha Uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani jijini Dar es Salaam.

Kituo hicho kina kiwanda cha ushonaji, kiwanda cha maji, chuo cha ufundi, Shule ya Sekondari Jitegemee na kumbi mbili za mikutano.

“Mkuu wa Majeshi umeeleza kwamba mlikuwa na mradi wenu wa matrekta, mlifanya kazi nzuri ya kugawa katika maeneo mbalimbali lakini mpaka sasa mnadai Sh bilioni 38 na zilikuwa bilioni 40 lakini bado 38 hazijaletwa.

“Watu wamechukua matrekta na wamefanyia biashara lakini hawarudishi deni. Baadhi ya watu waliopewa haya matrekta, zipo taasisi za Serikali lakini zipo pia taasisi binafsi, lakini kwa taarifa nilizokuwa nazo baadhi ya akaunti za matrekta haya fedha zinaingia kwenye mifuko ya watu binafsi.

“Sasa ninawaomba na nitoe wito kwa wote waliochukua na wanaodaiwa madeni kwa kuchukua matrekta…mimi niwape mwezi mmoja baada ya mwezi wawe wamelipa.

“Baada ya muda huo kama hazijalipwa, vyombo vyote vya ulinzi na usalama vitumie nguvu na bahati nzuri na ninyi mna polisi na wao ndiyo wanajua kweli kuwanyoosha kama mafua hayajatoka yatatoka.

“Kukopa harusi kulipa matanga, sasa mimi nataka kukopa iwe harusi na kulipa iwe harusi. Viwaanzie kuwasaka hawa wote Sh bilioni 38 ziweze kupatikana, ziweze kutumika kuanzisha viwanda vingine ili kusudi wasihangaike hawa tena kuniomba hela.

Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles