NEW YORK, Marekani
STAA Kim Kardashian, amesema kwamba, hakutaka kumpa jina la Chicago mwanawe, badala yake alitaka kumbatiza la bibi yake.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 37 na mumewe, Kanye, walimbatiza mtoto huyo Januari 15, mwaka huu baada ya kuibuka mvutano kuhusu jina.
Mbali na mtoto huyo, Kim na Kanye, wana watoto wengine wawili ambao mkubwa wa kike ana umri wa miaka minne anayeitwa North na wa kiume, Saint.
Akizungumza katika kipindi maalumu, staa huyo alisema tayari alikuwa ameshachagua majina mawili kabla ya kumpachika jina hilo.
“Nilitaka kumwita Jo kwa sababu ya bibi yangu Mary Jo ama Grace, lakini baadaye ndio tukaafikiana kumwita Chicago,” alisema nyota huyo katika mahojiano hayo.