Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamiii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameagiza waganga wakuu wa mikoa, wilaya na wafawidhi kuweka matangazo katika vituo vya afya, zahanati na hospitali kuhusu huduma za upimaji wa malaria kwamba ni bure.
Agizo hilo alilitoa jana mkoani Kigoma katika Zahanati ya Mwandiga wakati akizindua ugawaji wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu kwa wajawazito na watoto wenye umri wa mwaka mmoja.
Msaada huo umetolewa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania kupitia wizara ya afya kitengo cha kudhiti malaria   na Shirika la Misaada la Watu wa Marekani (USAID).
Ummy pia alipokea malalamiko ya wananchi wakidai kutozwa fedha kwa ajili ya matibabu wakati serikali imeagiza yawe bure.
Alisema ugawaji endelevu wa vyandarua ni mradi unaoendeshwa kwa pamoja na Shirika la Johns Hopkins kupitia Mradi wa VectorWorks kwa ufadhili wa USAID kupitia mfuko wa Rais wa Marekani wa kudhibiti malaria.
Waziri   alisema Ofisi ya Takwimu (NBS) mwaka 2017 zilionyesha kupungua kwa kiwango cha maambukizi ya malaria hadi chini ya asilimia 10 kutokana na mikakati iliyowekwa na wizara kuhakikisha wanatokomeza ugonjwa huo.
“Niendelee kusisitiza dawa za malaria na matibabu ni bure, wananchi hawatakiwi kulipia, wafadhili wetu wanajitoa sana kuhakikisha malaria inaisha.
“Waganga wafawidhi wanatuangusha sana niombe muweke matangazo na namba za simu kwenye vituo vya afya  wananchi watakaolipishwa watoe malalamiko yao,” alisema Ummy.
Mwakilishi wa USAID Tanzania, Andy Karas alisema kwa miaka zaidi ya 12 wamefanya kazi ya kupambana na malaria kupitia Mfuko wa Rais wa Marekani wa kupambana na malaria ujulikanao kama PM