25 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

‘KESI YA SCORPION YAPIGWA KALENDA’

FARAJA MASINDE -DAR ES SALAAM

KESI ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kujeruhi ikiwamo kumtoboa macho Said Mrisho, inayomkabili, Salum Njwete (34) maarufu ‘Scorpion’, imeahirishwa hadi Septemba 28, mwaka huu.

Kesi hiyo ambayo ipo katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala   Dar es Salaam, iliahirishwa jana na Hakimu Mkazi, Flora Haule kwa kuongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Nassoro Katuga baada ya Wakili wa Mtuhumiwa, Juma Nassoro kuwa nje kwa kazi.

“Shauri hili linakuja kwa ajili ya utetezi upande wa waleta maombi kwenye kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi.

“Hata hivyo Wakili wa mshatakiwa, Juma Nassoro yuko nje ya mahakama,  amesafiri yuko mkoni Arusha  hivyo naomba tarehe nyingine,” alidai Katuga.

Hakimu Haule alikubali maombi hayo ya upande wa mashtaka na kuahirisha kesi hadi Septemba 28, mwaka huu.

Upande huo wa utetezi ulifungua kesi hiyo ndogo ndani ya kesi ya msingi kutokana na kile ilichodai kuwa ‘Scorpion’ alilazimishwa kutoa maelezo kwa nguvu katika kituo cha polisi Buguruni.

Jambo hilo lilipingwa na shahidi namba tisa, Dc Bryson ambaye alidai kuwa alifanya mahojiano na mtuhumiwa kwa amani na kwa uhuru.

Hoja nyingine ambayo iliwasilishwa na upande huo wa utetezi ilikuwa ni kupinga mahakama kupokea maelezo yaliyowasilishwa na shahidi aliyemfanyia mahojiano Scorpion kwa madai kuwa yalikiuka kanuni na hivyo kuzuia mahakama hiyo kuyapokea kama kielelezo.

Hata hivyo mahakama hiyo ilidai kuwa kwa mujibu wa sheria, maelezo hayo yalikuwa hayajakiuka sheria kama ilivyodaiwa na upande wa waleta maombi na hivyo Mahakama hiyo ikayatambua.

Shahidi huyo akitoa ushahidi wake Agosti 8 mwaka huu kwa kuongozwa na  Wakili, Katuga,   alidai  wakati akifanya mahojiano na mtuhumiwa kituo cha polisi Buguruni, mtuhumiwa alitoa maelezo kwa uhuru na amani pasipo kushurutishwa.

“Mtuhumiwa alitoa maelezo kwa amani bila vurugu kinyume na inavyodaiwa na upande wa utetezi kuwa aliyatoa kwa kushurutishwa na kuteswa,” alisema Shahidi.

Katika hati ya mashtaka, ilidaiwa kuwa  Septemba 6,  mwaka jana saa 4 usiku maeneo ya Buguruni Sheli Wilaya ya Ilala Dar es Salaam, aliiba mkufu  wenye uzito wa gramu 34  na thamani ya Sh 60,000 na black bendi ya mkononi   na  Sh 330,000, vyote vikiwa na thamani ya Sh 474,000, mali ya Said Mrisho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles