33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

WAKULIMA WA MBAAZI WALALAMIKIA SOKO

Na BEATRICE MOSSES-MANYARA

WAKULIMA wa mbaazi katika Kijiji cha Malangi, Wilaya ya Babati mkoani Manyara, wamelalamikia kushuka kwa bei ya zao hilo.Wakizungumza na waandishi wa habari jana, wakulima hao walisema kwa sasa wanauza kilo moja ya mbaazi kwa Sh 400 badala ya Sh 1200 hadi Sh 2000 walizokuwa wakiuza miaka michache iliyopita.

Mmoja wa wakulima hao, Parmena Nnko, alisema kama hatua za haraka hazitachukuliwa, kuna uwezekano zao hilo likapotea kwa kuwa hawawezi kuendelea kupata hasara katika zao wanalolitegemea kibiashara.

“Serikali ilitutaka tulime kwa wingi zao hilo na kuahidi kuna wanunuzi kutoka nje ya nchi. Pamoja na kutoa ahadi hiyo, hadi sasa hakuna wanunuzi wowote kutoka nje na tunalazimika kuwauzia wanunuzi wa mitaani kwa bei ya hasara.

“Yaani, hata ukienda mjini unakuta bei wanayonunulia ni sawa na wanayonunulia hapa kijijini ndiyo maana mtu unaamua kuuzia hapa kijijini ili kuepuka gharama za usafiri.

“Kwa hiyo, tunaomba Serikali ichukue hatua za haraka ili kunusuru zao hilo kabla wananchi hawajakata tamaa,” alisema mwananchi huyo kwa niaba ya wenzake.

Naye Ofisa Biashara Mkoa wa Manyara, Ally Mokiwa, alikiri kuwapo kwa tatizo la bei kwa zao na kusema Serikali ya Mkoa wa Manyara inaangalia uwezekano wa kufungua kiwanda cha zao hilo badala ya kuwategemea wanunuzi kutoka nje ya nchi.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles