27.1 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

DIWANI ALALAMIKIWA MBELE YA MBUNGE

Na OSCAR ASSENGA-TANGA

 

BAADHI ya wakazi wa Mtaa wa Kichangani, Kata ya Maweni jijini Tanga, wamemlalamikia Diwani wa Kata ya Maweni, Joseph Calves (CCM), kwamba hashiriki shughuli za maendeleo.

 

Wakazi hao walitoa malalamiko hayo jana mbele ya Mbunge wa Tanga, Mussa Mbaruku (CUF), alipokuwa akizungumza nao na kushiriki uchimbaji wa mtaro wa kuwekea mabomba kwa ajili ya maji safi.

 

Akizungumza kwa niaba ya wananchi hao, Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Kichangani, Khatibu Mohamed, alisema wanashangazwa na kitendo cha diwani wao kushindwa kushirikiana nao katika shughuli za maendeleo kwa kuwa tabia hiyo inarudisha nyuma maendeleo yao.

“Tangu tulipoanza kuweka mipango ya kuchimba mtaro huu, baadhi ya viongozi wetu akiwamo huyo diwani, wamekuwa wakishindwa kushiriki uchimbaji huo na badala yake wananchi pekee ndio wanaojitokeza,” alisema Mohamed.

 

Akizungumzia malalamiko hayo, Mbunge Mbaruku alisema suala la kushiriki

maendeleo ya wananchi linahitaji ushirikiano wa pande zote bila kuangalia tofauti za kisiasa.

 

“Tunapozungumzia suala la maendeleo, lazima tushirikiane kwa pamoja kwa kuweka tofauti zetu za kisiasa pembeni.

 

“Kwa hiyo, mimi nitakuwa na nyinyi katika kazi hii na nitalipia gharama za chakula, maji ya kunywa na vifaa vya kuchimbia ili zoezi liweze kufanyika kwa wakati,” alisema mbunge huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,717FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles