27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, December 7, 2023

Contact us: [email protected]

MAHAKAMA YAWAONYA MAWAKILI WA SERIKALI

Na JANETH MUSHI-ARUSHA

MAHAKAMA ya Wilaya ya Arumeru, Mkoa wa Arusha, imewaonya mawakili wa upande wa Jamhuri katika kesi inayowakabili mmiliki wa Shule ya Lucky Vincent ya jijini Arusha, Innocent Mushi na Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule hiyo, Longino Nkana.

Mushi na Nkana wanakabiliwa na mashtaka ya usalama barabarani ikiwamo kusafirisha watoto bila kuwa na vibali muhimu.

Onyo hilo lilitolewa jana mahakamani hapo na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Desderi Kamugisha, baada ya wakili wa Jamhuri, Khalili Nuda, kudai mahakamani hapo kuwa hawajamaliza kuandaa hoja za awali kwa ajili ya kuwasomea washtakiwa.

Watuhumiwa hao walifunguliwa kesi namba 78 ya mwaka huu, katika Mahakama ya Wilaya ya Arumeru, wakikabiliwa na makosa ya usalama barabarani.

Katika maelezo yake, Hakimu Kamugisha alilazimika kuahirisha shauri hilo huku akisema hiyo ni mara ya mwisho kuahirisha shauri hilo kabla hajaamua kuchukua uamuzi mwingine.

“Rekodi za mahakama zinaonyesha kesi hii ililetwa kwa mara ya kwanza Mei 12, mwaka huu na upelelezi ulishakamilika.

“Kwa hiyo, naahirisha kwa mara ya mwisho hadi Septemba 11, mwaka huu na kama upande wa Jamhuri mtakuwa hamjakamilisha hoja hizo, mahakama itachukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria,” alisema Hakimu Kamugisha.

Awali, Wakili Nuda aliiomba mahakama hiyo kuahirisha kesi hiyo kutokana na kutokamilisha hoja hizo kwa ajili ya kuwasomea washtakiwa hao.

“Leo (jana), tulipanga kuwasomea hoja za awali ila hoja hizo hazijaandaliwa ipasavyo kwa upande wetu. Kwa hiyo, tunaomba tarehe fupi kwa ajili ya kuwasomea hoja hizo,” alidai Wakili Nuda.

 

Kwa upande wake, Wakili wa Utetezi, Method Kimomogoro, aliiambia mahakama hiyo kuwa hana pingamizi ila anaiomba mahakama hiyo itoe ahirisho la mwisho kwa upande wa jamhuri.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles