25.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

WALIMU WAKUU WAASWA KUJALI ELIMU YA AWALI

NA MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM



WAMILIKI na wakuu wa shule za awali wameshauriwa kufuatilia kwa karibu walimu wao wanaofundisha watoto wadogo ili masomo wanayofundishwa yaendane na umri wao.

Mbali na hayo, wakuu wa shule wameshauriwa kufuata misingi na utaratibu uliowekwa na Serikali wa kushirikisha walimu, wazazi na kamati ya shule ili kuzifanya shule hizo kuwa za jamii, badala ya kuwa za mfukoni.

Ushauri huo ulitolewa na Mratibu na Mkufunzi wa wa Taasisi ya kutetea haki za watoto Tanzania, Kelvin Shola, wakati wa kongamano lililohusisha walimu wa shule za awali kuhusu mtaala mpya wa shule hizo uliotolewa na Serikali, ambapo aliongeza kuwa, ili shule ya awali iweze kujipatia uhalali wa kutoa huduma, lazima iwe na vipengele hivyo vinne.

Alisema sifa kuu ya mwalimu wa awali ni kuwa karibu na watoto muda wote, kwa sababu kulingana na umri wao, wanaweza kuumizana na hatimaye baadhi yao wanaweza kuichukia shule.

“Baadhi ya walimu hawajui namna ya kuandaa watoto wadogo kabla ya kuanza elimu ya msingi, mwalimu wa awali lazima afundishe watoto kwa kumfikia mmoja mmoja ili kufahamu uelewa wao kwa karibu, kwakuwa elimu ya awali ndiyo kitovu cha elimu zote, ikikosewa ni tatizo kubwa,” alisema Shola.

Naye mwalimu wa shule ya awali kutoka Shule ya Msingi Ukombozi, Tunu Rashidi, alishauri panapotokea semina za mtaala huo mpya walimu wakuu wawapeleke walimu wanaohusika na watoto.

“Kuna changamoto kubwa, baadhi ya walimu wakuu hawapeleki walimu wahusika katika semina kama hizi za kuwajengea uwezo walimu wa awali, matokeo yake wanakwenda wasiohusika na kusababisha ujuzi huo kupotea.

“Semina za mitaala mipya, hususan ile ya kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK) zinafundisha mambo mengi, ikiwa ni pamoja na maelezo ya vitabu vipya, idadi ya vipindi kwa wiki na namna ya kuwafundisha, kwa kuwapanga kulingana na umri wao, vitu hivi vyote wanapaswa kuvipata wahusika moja kwa moja,” alisema Tunu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles