MAKINDA AZITAKA HOSPITALI KUJIUNGA NA NHIF

0
795
Mkuu wa Idara ya Masoko wa Kiwanda cha AfriTea and Coffee Blenders (1963) Ltd, Zachy Mbenna, akimwonyesha bidhaa zinazozalishwa na kiwanda hicho Spika mstaafu, Anne Makinda, alipotembelea banda lao katika Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, Dar es Salaam jana. Picha na Deus Mhagale.

MWENYEKITI wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda, amezitaka hospitali za Serikali kujiunga na huduma za matibabu yatolewayo na mfuko huo, ili wananchi wapate uhakika wa matibabu, hasa waishio vijijini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, Makinda alisema, hospitali za binafsi zinazotoa huduma za NHIF ni nyingi ukilinganisha na za Serikali.

Alisema hadi sasa hospitali zilizounganishwa na huduma za NHIF ni 6,998, ambapo hospitali za binafsi ni nyingi kuliko za Serikali.

“Nashauri hospitali za Serikali ambazo hazijajiunga na huduma hii wajiunge, kwa sababu kuna faida ya kupata mikopo ya vifaa tiba na dawa,” alisema Anne.

Alisema kuhusu Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), kwa sasa wamepanga kuongeza wigo ambapo mwanachama badala ya kutibiwa wilayani kwake atapata fursa ya kutibiwa hata mkoani.

Anne alisema usumbufu wa wazazi kulalamikia, matibabu ya watoto wao utakoma baada ya kujiunga na mfumo wa bima ya wanafunzi.

Katika maonyesho hayo, NHIF wamefanikiwa kuandikisha watoto zaidi ya 1,300 ambao wamejiunga na mfumo wa Toto Afya Kadi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here