Na Mwandishi Wetu
Kampuni ya Acacia Mining imesema kuwa itagharimu kiasi cha dola za Marekani milioni 30 kuweka mgodi wa Bulyanhulu katika matunzo na matengenezo baada ya Serikali kuzuia usafirishaji wa mchanga wa madini kuuza nje.
Acacia kwa sasa inapoteza dola milioni 15 kwa mwezi tangu kusitisha kwa usafirishaji wa mchanga wa madini mwezi Machi mwaka huu.
Kwa mujibu wa mtandao wa Weekly Mining unasema Mkurungezi Mkuu wa Acacia, Brad Gordon amesema itagharimu dola milioni 30 kufunga mgodi wa Bulyanhulu kwa kusitisha ajira na kuvunja mikataba kwa kiasi cha kati ya dola milioni 2 na 3 kwa mwezi katika utunzaji na gharama za matengenezo kwa kila mwezi.
Rais Magufuli alimtimua waziri wa Nishati na Madini pamoja na kuvunja bodi ya TMAA kutokana na ripoti ya Tume ya Mruma iliyochunguza makanikia ya madini yasafirishwayo nje na kampuni ya ACACIA .
Matokeo ya Tuem kuonekna alama za wizi na udanganyifu mkubwa wa ndani ya makotena yaliyozuiwa bandarini na serikali.
Ripoti ya pili ya ukaguzi ya Acacia bado inaendelea kusubiriwa baada ya kwanza kugundua kuwa makotena ya madini ya mchanga kuwa na kiwango cha mara 10 ya dhahabu tofauti na kilichotangazwa na kampuni hiyo, pia madini ya chuma na salfa ambayo kampuni hiyo haikutaja.
Acacia ilikanusha taarifa hiyo na kudai kuwa ripoti hawajaiona na kama kuna madini mengine kwao hayana thamani ya kibiashra.
"Kama sisi tukihakiki katika ripoti ya pili ambapo tunaona msuguano katika mazungumzo na serikali basi tunataka kuweka mgodi wa Bulyanhulu katika utunzaji na matengenezo," alisema Gordon.
Kusitisha kwa mchanga wa madini umeathiri shughuli za mgodi wa Bulyanhulu ambao ni mkubwa pamoja na gharama ya uendeshaji kubwa.
Kwa mujibu wa Acacia mgodi wa Buzwagi inakaridia katika kuisha muda wake wa uchimbaji, na kampuni inasemekana kwamba uzalishaji kwa mwaka huu itakuwa kati ya wakia 850 000 hadi 900 000.
Gordon alisema kuwa aliongozana mwenyekiti wa Acacia na Rais wa Barrick, Kelvin Dunshnisky katika ziara yake nchini katika jitihada za kutafuta suluhu.
Tangu kamati ya wataalamu wa sayansi iliyoundwa kuchunguza kiwango cha madini katika mchanga uliohifadhiwa katika makontena 277 yaliyoko bandarini Dar es Salaam, iwasilishe ripoti yake, kumekuwapo na sintofahamu ya kujua nani mkweli katika sakata hili kwa maana ya Serikali ya Tanzania kwa upande mmoja na wawekezaji Kampuni ya Acacia kwa upande mwingine.
Wakati ripoti iliyowasilishwa kwa Rais Dk. John Magufuli ikionyesha kuwa kiwango cha madini kinachosafirishwa nje ya nchi ni mara kumi zaidi, ikilinganishwa na kile ambacho kimekuwa kikielezwa, Acacia katika matamko yao mawili waliyoyatoa wiki hii imepinga ripoti hiyo.
Acacia inadai kuwa kama kiwango hicho kinachosemwa katika ripoti ya kamati hiyo ni kweli, basi Tanzania ni nchi inayoongoza duniani kwa kuwa na kiwango kikubwa cha madini ya dhahabu.
Katika tamko lake la mwanzo, Acacia ambayo inachimba madini katika migodi mikubwa ya Bulyanhulu na Buzwagi, ilieleza kuwa katika kila kontena la mchanga kuna madini ya shaba kilogramu 3,000, dhahabu kilo 3, na madini ya fedha kilo 3 na hivyo kufanya thamani ya kontena moja kuwa ni Sh milioni 300.
Katika ripoti ya Kamati ya Rais Magufuli, inaeleza kuwa katika makontena yote 277 yaliyochunguzwa dhahabu ilikuwa na uzito wa kati ya tani 7.8 na 13.16 zenye thamani kati ya Sh bilioni 676 na trilioni 1.147.
Kiwango hicho ni tofauti na makadirio ya wazalishaji na Wakala wa Serikali wa Ukaguzi wa Madini (TMAA) ambao walionyesha kuwa katika makontena hayo, dhahabu ilikuwa ni tani 1.2 yenye thamani ya Sh bilioni 97.5 tu.
Kwa upande wa madini mengine kama fedha, katika ripoti aliyokabidhiwa Rais Magufuli ilikuwa ni kati ya tani 1.7 na 1.9 yenye thamani kati ya Sh bilioni 2.1 na bilioni 2.4 wakati TMAA ikidai ni kg 831 zenye thamani ya Sh bilioni moja.
Kuhusu madini ya shaba, kamati hiyo ilibaini kulikuwa na tani 1,440.4 na 1,871.4 zenye thamani ya Sh bilioni 17.9 na bilioni 23.3.
Kiwango hicho ni tofauti na nyaraka zilizopatikana bandarini ambazo zilionyesha kulikuwa na tani 1,108 zenye thamani ya Sh bilioni 13.6.
Mwinda awa mwindwa
Bunge la Tanzania limegawanyika kuhusu ripoti hiyo na nini kifanyike na kutaka kutoa msimamo baada ya ripoti ya pili ya uchumi na sheria. Hivi basi sual hili limewekwa kiporo.
Kinachozua maswali na pengine baadhi sasa kuanza kuona kwamba hatima ya sakata hilo ni mapema mno kujua mwisho wake, ni kitendo cha wadau mbalimbali nao kuhoji uthabiti wa ripoti iliyowasilishwa kwa Rais Magufuli.
Kwa upande wa Acacia ilisema ripoti kuhusu mchanga wa dhahabu aliyopewa Rais John Magufuli ilijaa upotoshaji wa hali ya juu na imependekeza kufanyika kwa uchunguzi mpya ambao ni huru ili kuweza kupata ukweli.
Katika taarifa yake Acacia, yenye makao makuu jijini London, Uingereza, ilisema kwamba, ilijaribu mara kadhaa kuomba nakala ya ripoti hiyo nzima pamoja na utaratibu wa kuchukua sampuli kwenye uchunguzi huo, lakini mpaka sasa haijapewa.
“Kwa kuzingatia data tulizo nazo kwa zaidi ya miaka 20 ambazo tunaweza kuzitoa kwa ajili ya uchunguzi zaidi, hatuwezi kukubaliana na matokeo ya Tume. Data hizi ni data ambazo zimechambuliwa na kuandaliwa na Watanzania, wataalamu pamoja na taasisi za kimataifa na zimekuja na matokeo yanayofanana.
“Data hizi huru ambazo zinaweza kuthibitika zimeonyesha kuwa dhahabu kwenye mchanga ni chini ya asilimia moja ya kumi ya kiwango ambacho kimetajwa na ripoti ya tume. Kama data za ripoti ya tume zingekuwa kweli, Bulyanhulu na Buzwagi zingekuwa ndiyo wazalishaji wakubwa wa dhahabu duniani. Kutokana na upotoshaji huu, tunaamini tathmini mpya ambayo ni huru inahitajika,” inasomeka sehema ya Acacia kwa umma.
Zaidi ripoti hiyo inaeleza kuwa, Acacia imekuwa ikilipa mrahaba ambao ni asilimia 4 kwa mujibu wa makubaliano kati yake na Serikali pamoja na sheria za Tanzania na kuongeza kuwa, pamoja na kuwa kweli kuna baadhi ya aina nyingine za madini kama chuma, sulphur, rhodium na mengineyo kwenye mchanga, aina hizo hazina thamani kibiashara na kampuni hiyo haipati mapato yoyote kutokana nayo.