26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

MAREKANI YAMWEKEA VIKWAZO MSHAURI WA KABILA

WASHINGTON, MAREKANI


SERIKALI ya Marekani imemwekea vikwazo mshauri mkuu wa Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Aidha imeiongezea shinikizo Serikali ya Kabila kuhusu kuchelewesha uchaguzi na madai ya ukiukaji wa haki za binadamu.

Hatua hiyo inafuatia tangazo lililotolewa na Umoja wa Ulaya (EU) la kuwawekea vikwazo vya usafiri na kuwafungia mali zao raia tisa wa DRC, hiyo ikiwa ni moja ya njia za kuishinikiza Serikali kuandaa uchaguzi kumchagua atakayeichukua nafasi ya Kabila kabla mwishoni mwa mwaka.

Wizara ya Fedha ya Marekani ilimweka Jenerali Francois Olenga katika orodha maalumu ya watu, na kukamata mali yoyote aliyonayo hapa na kuwazuia Wamarekani kujihusisha naye katika biashara ya aina yoyote.

Katika taarifa yake, wizara hiyo ilisema Olenga Olenga ambaye alipigana pamoja na baba yake Kabila, marehemu Laurent Kabila katika vita vilivyomwondoa madarakani dikteta Mobutu Sese Seko mwaka 1997, anasimamia kikosi cha walinzi kinachotishia wale wanaomkosoa Kabila na kuwakamata na hata kuwaua raia wa DRC.

Serikali ya DRC imekanusha kwamba inatumia nguvu kupita kiasi dhidi ya raia wake.

Aidha Olenga na msemaji wa jeshi la DRC hawakupatikana kwa wakati kujibu tuhuma hizo na kuhusu vikwazo hivyo vipya. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles