27.2 C
Dar es Salaam
Monday, January 20, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Wanafunzi Udsm wahamasishwa kusoma vitabu kujifunza maendeleo ya China

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wametakiwa kusoma vitabu mbalimbali kutoka China kikiwemo kinachozungumzia dhana ya utawala bora ili kujifunza namna nchi hiyo ilivyoendelea.

Ushauri huo umetolewa Desemba 11,2024 na Mkurugenzi Mtanzania wa Taasisi ya Confucius Chuo Kikuu cha Dar es Salaam inayofundisha lugha ya Kichina, Profesa Aldin Mutembei, wakati wa hafla ya kupokea vitabu vilivyotolewa na Kampuni ya Ujenzi na Mawasiliano ya China (CCCC) kwa ajili ya chuo hicho.

Amesema kuna aina 43 za vitabu mbalimbali vinavyozungumzia maendeleo na utamaduni wa China ambavyo wanafunzi katika chuo hicho wanaweza kuvitumia kuongeza maarifa.

“Kuna aina 43 za vitabu mfano utawala bora, kujifunza dhana ya utawala bora kutoka mawazo ya China, juzuu zote nne wasome wajue kwanini China imeendelea, kuna kitabu kinachozungumzia mtandao wa China uliowawezesha kutoka walikokuwa zaidi ya miaka 1800.

“Kuna dhana mpya ambayo inafanya China iweze kuwasiliana na dunia nzima katika diplomasia ya lugha na kujenga uchumi, kuna vitabu vya Kemia na mada 100 zinazohusu vijana na utamaduni…kuna kitabu kinachoeleza kujua faida ya kucheka, kwanini kucheka ni afya,” amesema Profesa Mutembei.

Naye Kaimu Mkurugenzi Huduma za Maktaba Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Collin Kimaryo, amesema vitabu hivyo vitawafaa kwa sababu kazi yao ya msingi ni kutoa huduma ya machapisho mbalimbali.

“Mwaka jana tulipokea vitabu na mwaka huu tumepokea vitabu 200 vinahusu sanaa, historia, sayansi na teknolojia, tutaongeza idadi ya vitabu ambavyo wanafunzi na wasomaji wetu watakwenda kuvitumia kupata maarifa,” amesema Dk. Kimaryo.

Aidha amesema utoaji vitabu hivyo utazidi kudumisha ushirikiano uliopo baina ya chuo hicho na Kampuni ya CCCC pamoja na China na Tanzania.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Kampuni ya CCCC, Li Xuecai, amesema utoaji vitabu hivyo unalenga kuimarisha urafiki kati ya China na Tanzania na kubadilisha tamaduni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles