24.8 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

ARIANA GRANDE ALIYENUSURIKA KIFO

MWANAMUZIKI huyu wa kike, Ariana Grande, anayetamba na nyimbo mbalimbali, ukiwamo wa ‘Side To Side’ aliomshirikisha Nicki Minaj, amezaliwa Juni 26, 1993 huko Boca Raton, Florida, nchini Marekani.

Ni mwanamuziki na mwigizaji wa Marekani anayeshika namba mbili kwa kufuatiliwa zaidi kwenye mtandao wa Instagram.

Ariana alianza muziki huko Broadway akiwa na miaka 13 kabla hajaanza kuigiza nafasi ya Cat Valentine kwenye kipindi cha watoto kupitia Televisheni ya Nickelodeon mwaka 2009.

Alifanya kazi hiyo miaka minne kisha alijiunga na kipindi cha Sam & Cat hadi mwaka 2014, baada ya hapo amecheza michezo mbalimbali ya kuigiza jukwaani, ameigiza katika filamu mbalimbali na vipindi mbalimbali vya runinga, huku sauti yake ikitumika kuigiza sauti za wanyama kwenye vipindi mbalimbali vya televisheni.

Alianza kwa wimbo wa ‘Soundtrack’ mwaka 2011, lakini baada ya hapo akaingia mkataba na Kampuni ya Republic Records inayomsimamia kazi zake hadi sasa.

Albamu yake ya kwanza ya ‘Yours Truly’ ilitoka mwaka 2013, ambayo ilishika namba moja kwenye chati za Billboard, albamu ya pili aliyoiita ‘My Everything’ aliyoiachia mwaka 2014 nayo iliingia kwenye 10 bora kwenye chati hizo na chati za nchi mbalimbali ikiwa na nyimbo kama ‘Problem’, ‘Break Free’, ‘Bang Bang’ na ‘Love Me Harder’.

Mwaka 2015, Grande aliitangaza albamu yake ya ‘My Everything’ kwenye ziara yake ya kwanza tangu alipoanza muziki wake aliyoiita ‘The Honeymoon Tour’.

Mwaka 2016 aliachia albamu yake ya tatu aliyoiita, ‘Dangerous Woman’, yenye wimbo ‘The title track’ ulioshika namba 10 kwenye nyimbo kali 100 za Billboard.

Wimbo huo ulimpa nafasi ya kuwa mwanamuziki wa kwanza kwenye historia ya muziki kuwa na nyimbo tatu kutoka kwenye albamu zake tatu zikiwa zinafanya vizuri katika chati hizo. Hadi Januari video zake mitandaoni ziliangaliwa na watu zaidi ya bilioni saba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles