26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

DAVIDO ‘KUUA’ SHABIKI WA KIKE NIGERIA

LAGOS, NIGERIA


KAMA utani, lakini ndiyo ukweli wenyewe kutoka kwa shabiki wa kike wa msanii wa muziki nchini Nigeria, David Adeleke, kutangaza kujiua ifikapo Agosti 13, mwaka huu, kama atashindwa kuonana na msanii huyo.

Shabiki huyo wa kike, ambaye hakutaka jina lake lijulikane, amesambaza video yake kwenye mitandao ya kijamii akitangaza kuwa yupo tayari kujiua endapo atashindwa kuonana na Davido kabla ya tarehe yake hiyo ya kuzaliwa.

“Davido, Agosti 13 ni siku yangu ya kuzaliwa, hivyo kuanzia leo kama nitashindwa kuonana na Davido kwa macho yangu hadi kufikia siku hiyo ya kuzaliwa kwangu, basi lazima nijiue, ili kuokoa maisha yangu naomba nionane na Davido nipate furaha moyoni mwangu.

“Nimekuwa nikimfuatilia tangu 2014 kupitia akaunti yake ya Twitter, Instagram na Facebook, lakini hataki kunijibu chochote, mimi ni shabiki wake namba moja, lakini kwa kuwa hataki nimuone basi nataka kujiua kwa ajili yake,” alisema mrembo huyo kupitia video aliyojirekodi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles