23.9 C
Dar es Salaam
Friday, May 27, 2022

NAMELESS: WIVU UTANIWEKA PABAYA

NAIROBI, KENYA


MSANII anayetamba na wimbo wa ‘Sinzia’, David Mathenge, maarufu kwa jina la Nameless, ameweka wazi kuwa wivu wake unaweza kumuweka pabaya.

Kauli hiyo aliitoa baada ya kuchukizwa na DJ Kym Nick Dee wa kituo cha runinga cha Kiss TV nchini humo alipomkumbatia mke wake ambaye ni mwimbaji mwenzake, Wahu Kagwi.

DJ huyo aliposti picha akiwa na Wahu wakiwa wamekumbatiana baada ya kumalizika mahojiano yao.

Baada ya Nameless kuiona picha hiyo kwenye mitandao, alianza kutoa vitisho kwa Dj huyo, huku akionesha kuchukizwa na hiyo picha.

“Hata kama walikuwa kwenye kipindi, lakini wanatakiwa kujua kwamba Wahu ni mke wa mtu, huwezi kuamua kumkumbatia na baadaye unatuma picha kwenye mitandao ya kijamii, namchukia sana na ninaamini wivu wangu unaweza kuniweka pabaya siku moja,” aliandika Nameless.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,432FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles