24.8 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

LIVERPOOL YASOGEA NAFASI YA TATU

LONDON, ENGLAND


LIGI Kuu nchini England iliendelea jana kwenye viwanja mbalimbali, huku Liverpool ikishinda bao 1-0 mbele ya wapinzani wao West Brom.

Mchezo huo ulionekana kuwa na ushindani wa hali ya juu, huku West Brom wakipambana kuhakikisha inashinda kwenye uwanja wa nyumbani na kuwafurahisha mashabiki wao.

West Brom walianza kwa kucheza mipira ya mbali ambapo dakika ya pili walipata nafasi, lakini walishindwa kuitumia huku walinzi wa Liverpool wakionesha kuwa imara na kuondoa mpira huo wa hatari.

Kuanzia dakika ya tatu hadi ya 10, Liverpool walionekana kutafuta bao la mapema lakini ukuta wa West Brom ulionekana kuwa imara kwa dakika hizo.

Dakika ya 15 na 24 Liverpool walipata nafasi za wazi lakini walishindwa kuzitumia hadi kumfanya kocha wao, Jurgen Klopp, kuinuka kwenye kiti na kuanza kuwapanga wachezaji wake.

Dakika ya 45 Liverpool walifanikiwa kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wao, Roberto Firmino, baada ya kazi nzuri ambayo ilifanywa na Lucas Pezzini-Leiva.

Baada ya kipindi cha pili kuanza, wenyeji West Brom walionekana kubadilika na kutafuta bao la kusawazisha, huku wakifanya mabadiliko kwa baadhi ya wachezaji wao lakini bado hali ilionekana kuwa ngumu.

Dakika ya 82, Liverpool walionekana kushindwa kuongeza kasi ya mashambulizi hivyo waliamua kufanya mabadiliko, huku akiingia Daniel Sturridge kuchukua nafasi ya Divock Okoth Origi lakini bado ukuta wa West Brom ulionekana kuwa imara.

Dakika ya 90, Liverpool walionekana kuwa na dalili za kupoteza muda, hivyo walifanya mabadiliko ambapo aliingia Alberto Pérez kuchukua nafasi ya kiungo mshambuliaji, Philippe Coutinho, hata hivyo mabadiliko hayo hayakuwa na madhara yoyote hadi mchezo huo unamalizika na kuifanya Liverpool ishike nafasi ya tatu ikiwa na pointi 66 baada ya kucheza michezo 33.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles