25.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 26, 2021

MASHABIKI WAMTAKA MOYES KUJIUZULU

LONDON, ENGLAND


BAADA ya klabu ya Sunderland kukubali sare ya mabao 2-2 dhidi ya West Ham juzi kwenye uwanja wa nyumbani, mashabiki wa timu hiyo wamemtaka kocha wao, David Moyes kujiuzulu.

Mashabiki hao waliamini kuwa kocha huyo atakuwa suluhisho la matatizo yao ndani ya klabu hiyo, lakini hadi sasa timu hiyo inashika nafasi ya 20 ambayo ni ya mwisho kwenye msimamo wa ligi, ikiwa imecheza michezo 32 na kupata pointi 21.

Timu hiyo kuna uwezekano mkubwa wa kushuka daraja msimu huu, hivyo mashabiki baada ya mchezo wa juzi dhidi ya West Ham kutoka sare, walionekana kumzomea na kumtaka aondoke awaachie timu yao.

Hata hivyo, kocha huyo wa zamani wa Everton na Manchester United, anaamini bado timu yake ina nafasi kubwa ya kufanya vizuri michezo iliyobaki kutokana na mabadiliko anayoyaona.

“Nimewaona mashabiki wakinizomea baada ya sare hiyo dhidi ya West Ham, nilitarajia kuona hali hiyo kutokana na timu kushindwa kufanya vizuri pamoja na kocha wake kwa kipindi cha siku za hivi karibuni.

“Natakiwa kukubaliana na hali hiyo kwa kuwa mashabiki wanataka kuona timu yao ikiwa inashinda na kupata pointi, nakumbuka nimewahi kufanya vizuri kwenye michuano ya ligi kuu na ndio maana mashabiki wa Sunderland wanashangaa kuona timu ipo katika hali hii kwa sasa.

“Najua mashabiki wapo pamoja na timu yao kuhakikisha inafanya vizuri, lakini ukweli ni kwamba kocha pamoja na wachezaji wake hatufanyi vizuri, hivyo tunastahili kutupiwa lawama hizo na si mtu mwingine.

“Lakini ninaamini katika mchezo dhidi ya West Ham tulionesha kiwango cha hali ya juu ila wenzetu walikuwa bora zaidi yetu, lakini bado tutahakikisha tunapambana ili kuiokoa timu kushuka daraja,” alisema Moyes.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,173FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles