24.1 C
Dar es Salaam
Thursday, October 21, 2021

MR. BLUE AGOMBEWA KWA SELFIE

RAPA Herry Sameer ‘Mr. Blue’, usiku wa jana aliikaribisha sikukuu ya Pasaka kwa shangwe kubwa kutoka kwa mashabiki wake wa Zanzibar waliokuwa na hamu ya kupiga naye picha ‘selfie’.

Mr. Blue alijikuta katika wakati huo mashabiki wake walipomuona akiwa nyuma ya jukwaa akijiandaa kwa shoo ya Zanzibar Swahili Festival iliyofanyika usiku wa kuamkia jana kwenye Ukumbi wa Ngome Kongwe visiwani Zanzibar.

Baadhi ya mashabiki wake walimsogelea mmoja mmoja wakiomba kupiga naye picha, lakini aliwataka wasubiri hadi alipomaliza shoo yake iliyokuwa na shagwe na nderemo za kila aina.

Baada ya shoo hiyo mashabiki hao waliongezeka baada ya kupeana taarifa kwamba Mr. Blue amekubali kupiga nao picha, walimzunguka na kisha kila mmoja alipiga naye picha kama walivyotaka.

Mr. Blue ametimiza miaka 30 baada ya juzi kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa, huku Young Killer naye alitimiza miaka kadhaa licha ya kufurahia tarehe na mwezi sawa wa kuzaliwa na Mr. Blue.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,644FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles