32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

MTOTO ALIYEANZA KUONGEA AKIWA NA MIEZI MINNE

Na JUSTIN DAMIAN


AKIPATA Shahada yake ya kwanza akiwa na umri wa miaka kumi, Michael Kearney siku zote alikuwa mbele ya muda. Mtoto huyu ambaye anaaminika kuwa ndiye mwenye uwezo mkubwa wa akili katika umri mdogo alianza kuongea akiwa na umri wa miezi minne tu.

Akiwa na umri wa miezi 10 alikuwa tayari anajua kusoma na akiwa na miaka minne aliweza kufanya vizuri kwenye mtihani wa majaribio wa Hisabati aliopewa.

Kwa mujibu wa wana saikolojia, watoto wa aina yake hutokea mara chache na kuna baadhi ya nchi au sehemu hawajawahi kutokea kabisa.

Michael Kearney alizaliwa mwaka 1984 huko Hawaii Marekani na ni mmoja wa watoto waliovunja rekodi ya dunia kwa kuwa na akili nyingi akifanikiwa kumaliza chuo kikuu katika umri mdogo pamoja na kufundisha chuo kikuu akiwa na umri mdogo kabisa.

Siku za mwanzo za maisha yake

Mtoto huyo alikuwa akijifunzia nyumbani huku akipata msaada kutoka kwa baba na mama yake ambaye alikuwa ni Mmarekani mwenye asili ya Japan. Dada yake aliyeitwa Maeghan naye aliweza kumaliza chuo kikuu akiwa na umri wa miaka 16 tu.

Kwa mujibu wa Profesa wa saikolojia Martha J. Morelock, Kearney alisaidiwa na wazazi wake kufahamu mambo mengi na alikuwa na uwezo wa pekee wa kuelewa.

Mtoto huyo alizungumza neno lake la kwanza akiwa na umri wa miezi minne. Akiwa na umri wa miezi sita aliweza kumwambia daktari wao “nina maumivu kwenye sikio langu la kushoto.”

Akiwa na umri wa miaka minne, alipewa jaribio la Hisabati na shule ya Hisabati ya Johns Hopkins bila kuwa amesoma kwa ajili ya mtihani na alifaulu kwa kiwango cha juu.

Alisoma katika shule ya San Marin High School iliyopo Novato huko California kwa mwaka mmoja na alimaliza akiwa na umri wa miaka sita mwaka 1990. Mwaka 1994 walikuwa wakishiriki kwenye kipindi maaraufu cha television kilichoitwa Tonight Show.

 

Elimu ya chuo

Alijiunga na shule ya Santa Rosa Junior College iliyopo Sonoma California na alimaliza akiwa na umri wa miaka minane akichukua masomo ya Sayansi ya madini. Mwaka 1993 familia yake ilihamia Alabama na alifanikiwa kuingia kwenye rekodi ya kitabu cha Guinness kuwa mtu mwenye umri mdogo zaidi duniani kumaliza chuo kikuu akiwa na miaka 10, akichukua Shahada ya Masuala ya kale.

 

Utafiti na kufundisha

Alimaliza Shahada yake ya pili (masters) ya Kemia kutoka chuo kikuu cha umma cha Tennessee huko Marekani akiwa na miaka 14. Utafiti wake aliofanya ili aweze kupata shahada hiyo ya pili uliokuwa na kurasa 118 uliwashangaza wengi na alivunja rekodi ya dunia kwa kuwa mtu wa kwanza mwenye umri mdogo kuweza kupata Shahada ya pili duniani.

Akiwa mdogo pia alijihusisha na onyesho la kwenye televisheni ambapo yeye na wazazi wake walihamia Hollywood kurekodi sehemu ya kwanza ya onyesho hilo ambalo hata hivyo halikufanya vizuri kama walivyotarajia.

Octoba 2006, aliweza kushinda shindano lingine la kwenye televisheni ambapo alipata Dola  za Marekani 100,000 (zaidi ya Sh milioni 200 za Kitanzania). 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles