26 C
Dar es Salaam
Friday, November 29, 2024

Contact us: [email protected]

PANGA LAFYEKA VIGOGO UHAMIAJI

Na Mwandishi Wetu-DARES SALAAM

KAMISHNA Jenerali wa Uhamiaji nchini, Dk. Anna Makakala, amefanya mabadiliko makubwa ya viongozi wa Idara ya Uhamiaji wa mikoa mbalimbali pamoja na kuwateua viongozi wapya wa mikoa kushika nyadhifa hizo kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar.

Katika mabadiliko hayo amewapangua vigogo waliokuwa mikoani na kwenda mikoa mingine kama inavyoonekana kwenye mabano, ambapo  Naibu Kamishna wa Uhamiaji Sixstus Nyaki (Mwanza) anakwenda Simiyu, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Selemani Kameya (Rukwa) anakwenda Tabora.

Mkuu wa Uhamiaji Naibu Kamishna wa Uhamiaji,  Asumsio  Achacha (Mbeya), amehamishiwa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mkuu wa Uhamiaji Naibu Kamishna, Peter Kundy (Manyara) anakwenda Dodoma kuchukua nafasi ya  Kamishna Msaidizi  Ali Mohamed ambaye amehamishiwa   Arusha. 

Taarifa hiyo ya Uhamiaji, ilieleza kwamba Naibu Kamishna wa Uhamiaji  Mkemi Seif  ameteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Kusini Unguja huku Naibu Kamishna wa Uhamiaji  Muhsin Abdallah Muhsin akiteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Naibu Kamishna wa Uhamiaji  Said Hamdani ameteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji  Mkoa wa Mjini Magharibi.

“Naibu Kamishna wa Uhamiaji Othman Khamis Salum  ameteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mjini Magharibi Unguja. Katika mabadiliko hayo baadhi ya Wakuu wa Uhamiaji wa mikoa wamebaki katika vituo vyao vya kazi vya awali akiwemo aliyekuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Morogoro Naibu Kamishna wa Safina Muhindi, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Lindi  na Naibu Kamishna wa Uhamiaji George Kombe anakuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma.

“Naibu Kamishna wa Uhamiaji Hilgaty Shauri, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Singida, Naibu Kamishna Faith Ihano  na Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Mara  Naibu Kamishna  Fredrick Eustace  Kiondo,” ilieleza taarifa hiyo.

Wengine waliobaki kwenye vituo vyao vya awali ni pamoja na  Naibu Kamishna Abdallah Towo (Kagera) na  Naibu Kamishna Anastazia  Ngatunga (Shinyanga).

Katika mabadiliko hayo Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dk. Makakala pia amewateua  viongozi wa uhamiaji wa mikoa  ambao ni Naibu Kamishna Mary Palmer (Dar es Salaam),  Naibu Kamishna Plasid  Mazengo(Pwani), Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji  James Mwanjotile(Mtwara),  Kamishna Msaidizi Mwandamizi  Hope Kawawa (Iringa),  na  Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji  Hosea Kagimbo  (Njombe).

Wengine ni Naibu Kamishna Rashid Magetta  (Songwe),  Naibu Kamishna Carlos Haule,  (Rukwa),  Naibu Kamishna Julieth Sagamiko (Manyara),  Naibu Kamishna  Albert Rwelamila (Kilimanjaro) na  Naibu Kamishna Paul Eranga (Mwanza). 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles