29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 20, 2021

BUNGE KUJADILI HALI YA UCHUMI

Na MWANDISHI WETU-DODOMA

MKUTANO wa saba wa Bunge unatarajia kuanza vikao vyake leo mjini Dodoma huku ukiwa mahususi kwa ajili ya kupitisha Bajeti ya serikali, pamoja na kujadili utekelezaji wa bajeti za wizara kwa mwaka 2016/17 na makadirio ya matumizi ya serikali kwa mwaka 2017/18.

Kabla ya uwasilishaji wa bajeti ya serikali, Bunge pia litajadili hotuba ya hali ya uchumi wa Taifa itakayowasilishwa bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano, Owen Mwandumbya mbali na shughuli hiyo pia kutakuwa na kiapo cha uaminifu cha Mbunge wa Kuteuliwa, Salma Kikwete.

“Kabla ya uwasilishwaji wa bajeti ya Serikali, Bunge litajadili hotuba ya hali uchumi wa Taifa itakayowasilishwa bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango,”alisema.

Alisema katika mkutano huo pia kutakuwepo na uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), ambao utafanyika leo kwa kuchagua wabunge tisa watakaoiwakilisha Tanzania katika Bunge hilo.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,594FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles