32.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

HONGERENI KWA KUPUNGUZA MZAHA BARABARANI

Na FARAJA MASINDE


MICHEZO na kukosa umakini barabarani ilikuwa ni tabia madereva wengi wa bodaboda hapa nchini.

Madereva hao walikuwa wakifanya fujo pindi wanapokuwapo barabarani, jambo ambalo lilikuwa likiwasababishia ajali kila kukicha.

Kero kubwa hasa ilikuwa ni kuendesha pikipiki huku wakiwa wameshika usukani mkono mmoja, kelele zinazotokana na kufungulia redio kwa nguvu pamoja na uendeshaji usiokuwa rafiki kwa watumiaji wengine wa barabara.

Hali hii ilikuwa ikiwafanya baadhi ya watu kuuchukia usafiri huu kutokana na fujo hizo zinazofanywa na vijana wachache wasiojali kazi yao.

Mkazo ambao umekuwa ukiwekwa na Jeshi la Polisi kwa kipindi kirefu sasa umesaidia kupunguza baadhi ya tabia hizi zilizokuwa zikihatarisha maisha yao na ya abiria.

Licha ya kuwa bado kuna baadhi ya vijana wanaendelea na tabia hizi zisizofurahisha, lakini ni dhahili kuwa kumekuwa na mafanikio makubwa kwani wengi sasa wamekuwa na utii wa sheria bila shuruti kufuatia kuogopwa kupigwa faini zisizokuwa za lazima ambazo zinaweza kuepukika.

Jambo hili licha ya kuwa na manufaa kwa abiria, pia limesaidia kupunguza ajali za mara kwa mara ambazo zilikuwa zikichangiwa hasa na kukosekana kwa umakini wa madereva hawa, yote haya huwa wanayafanya kwa madai ya kuwahi abiria.

Tabia nyingine ambayo si nzuri kwa madereva hawa ni ya kuendesha bodaboda huku wakisikiliza simu zao kwa kutumia ‘earphone’.

Kitendo hiki ambacho kilikuwa kinawapunguzia umakini barabarani, nacho kimepungua kwa kiasi kikubwa.

Ilikuwa si ajabu kuwakuta madereva hawa wakiwa wanaendesha kwa mwendo kasi huku wakisikiliza miziki kupitia simu zao za mkononi, hii ilikuwa ni kwa wale ambao hawajafunga redio katika pikipiki zao.

Madereva hawa ambao ni mahodari wa kusaka fedha na hawakatai abiria hata kama wamebeba mizigo inayozidi uwezo wa pikipiki, huwa hawawazi usalama wao hata kidogo.

Bila kujali amebeba abiria wa aina gani, vijana hawa hufungulia muziki mkubwa bila kujali kuwa wanakera watu wa pembeni yao.

Licha ya kukera watu,athari ya jambo hilo ni kupata ajali bila kutarajia. Hiini kwa sababu dereva anaweza kupigiwa honi ya kuashiria hatari na asisikie kutokana na sauti ya muziki.

George Otenga ni miongoni mwa watu wanaopenda kupanda bodaboda anasema kuwa tatizo kubwa linalowakabili vijana hawa  ni kutojitambua, ndio maana hata baadhi ya watu wanawadharau.

“Wanajua madhara ya kuweka ‘earphone’ masikioni, lakini wanadharau. Wacha waendelee kukamatwa na askari wa barabarani kwani jambo hililinahatarisha maisha ya watu wengi si tu wao.

“Mimi huwa napanda pikipiki lakini huwa naangalia nidhamu ya dereva, siwezi kujipandia tu. Unakuta dereva anaimba kuanzia mwanzo wa safari hadi mwisho. Mkipata dharura hata ukimwambia hakusikii hadi umshtue kwa kumvuta koti ndipo akusikilize,” anasema Otenga.

Hivyo, kuacha kupungua kwa tabia hii kumesaidia kuwafanya wawe makini barabarani. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles