33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

LISSU AWAPA MBINU MPYA VIJANA

Na LILIAN JUSTICE, MOROGORO


MWANASHERIA Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, amewapa mbinu vijana kwa ajili ya kuishi kwa amani katika Serikali ya Rais Dk. John Magufuli.

Amesema kwamba, ili vijana hao wasisumbuliwe na Serikali iliyoko madarakani, wanatakiwa kujua masuala mbalimbali ya kidunia na pia wasiwe waoga pindi wanapopigania haki katika masuala mbalimbali.

Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, aliyasema hayo juzi mjini hapa wakati akizungumza kwenye mkutano wa umoja wa wanachama wa chama hicho ambao ni wanafunzi wa vyuo vikuu.

“Sisi kama Chadema, hatutarudi nyuma katika mapambano mpaka tutakapochukua dola mwaka 2020.

“Ili tufikie malengo hayo, lazima vijana msiwe waoga, lazima mjue haki zenu na kupambanua mambo mbalimbali kwa sababu Serikali iliyoko madarakani inalenga kutudhoofisha wapinzani.

“Katika mfumo huu wa vyama vingi, ni vema Serikali ikatambua kuwa Chadema inapoikosoa Serikali, haina maana ya kuwachochea wananchi na badala yake inataka maisha ya wananchi yaboreshwe,” alisema Lissu.

Naye Mbunge wa Viti Maalumu wa Chama hicho, Devotha Minja, alisema vijana wengi wasomi wamekuwa wakishindwa kupata ajira kutokana na mfumo mbovu uliopo serikalini.

“Sasa basi, nawaomba vijana msikubali kudanganywa na baadhi ya wanasiasa wasioitakia mema nchi hii na badala yake muendeleze mshikamano bila kukata tamaa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Umoja huo uitwao CHASO, Jafar Ndege, alisema ni vema vijana wakawa chachu ya kuleta maendeleo katika Taifa kwani wanayo fursa kubwa ya kuibua mambo ya maendeleo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles