28.2 C
Dar es Salaam
Monday, December 2, 2024

Contact us: [email protected]

EMILY NIKOLS: MAMA ANAYEFANYAKAZI MAJUMBANI AKIWA MTUPU

NI mama wa mtoto mmoja aliye katika ndoa, ambaye kwa mtazamo wa haraka kutokana na sababu za kimaadili na heshima yake ungetarajia afanye kazi inayomstahi.

Lakini badala yake mama huyu, Emily Nikols (25) mwenye binti wa umri wa miezi tisa amechagua kazi ambayo ina mtazamo hasi. Yaani yenye kudhalilisha utu na heshima yake.

Lakini mwenyewe ana mawazo tofauti na hayo, kimtazamo kwake kazi hiyo ya kufanya usafi akiwa mtupu mbele ya macho ya wanaume ni sawa tu  na anaifurahia kwa sana.

Emily hulipwa Pauni 45 za Uingereza sawa na Sh 125,000 za Tanzania kufanya usafi wa nyumba nzima, kufua nguo na kupiga pasi akiwa mtupu kama alivyozaliwa.

Pamoja na kwamba hana tatizo iwapo mwanamume mwenye nyumba atakuwa amekaa akimkodolea macho kodo anapowajibika akiwa kama alivyozaliwa, wateja huwa hawaruhusiwi kumgusa wala kumtongoza.

Kwa mujibu wa ripoti, alianza kazi hiyo mwezi uliopita baada ya kujifungua binti wa kike miezi tisa iliyopita.

Fedha anazopata kwa kazi hiyo, anasema humsaidia mno nyumbani ikiwamo malezi ya bintiye na mumewe hana tatizo kuhusu kibarua hicho cha kushangaza.

Hata hivyo, imebainika kuwa hayuko peke yake katika biashara hiyo, kwani ni mwajiriwa wa Kampuni ya Naturist Cleaners iliyoajiri wanaume na wanawake 80, ambao hukodishwa kufanya kazi za nyumbani wakiwa watupu.

“Kila mtu ana utupu wake anaoficha ndani ya mavazi, sioni kwanini tunaogopa kuhusu hili,” anasema.

Kuhusu kutongozwa na wateja, anasema kwamba wateja wake wa kiume ni watu waungwana na hivyo hawamsumbui wala kumghasi kimapenzi.

Mkazi huyo wa Liverpool, anaendelea kusema: “Kwangu kufanya usafi nikiwa mtupu si jambo kubwa– ni kawaida mno!

“Mimi kwa kweli ni mtu mwenye kujiamini na ninajisikia vyema nikiwa mtupu na hivyo sijisikii vibaya au kuhisi hali ya udhalili.

 “Swali ninaloulizwa mara kwa mara na watu ni iwapo nasikia baridi, ukweli ni kwamba baada ya muda mchache nikiwa mtupu nikiwajibika nazoea hali ya hewa.

“Marafiki na dada zangu wananiunga mkono sambamba na mume wangu, ambaye awali alikuwa na wasiwasi wa usalama wangu, ananiamini mno. Mimi ni mtu mzima.

“Sifanyi ukahaba, niko huru na mwili wangu na wala sijali michirizi kadhaa mapajani au tumboni mwangu baada ya kujifungua.

Emily alipata kazi hiyo mpya baada ya rafiki yake kumwambia uwapo wa wanawake wanaolipwa wakichukuliwa video wakisafisha nyumba wakiwa watupu.

Aliiona kampuni hiyo, yaani Naturist Cleaners katika mtandao wa Google, ambayo anafanya kazi nayo miezi miwili sasa.

Emily anasema ameipenda kazi kwa sababu inamruhusu kujipatia fedha wakati akimlea bintiye mwenye umri wa miezi tisa.

Wafanyakazi wa usafi hulipwa pauni 45 kwa saa na wateja wao lazima waingie mkataba unaowakataza kuwashika shika au kuwatongoza.

Kutokana na kuwa watupu toka kichwani hadi chini wafanyakazi hawa wa usafi hawafanyi kazi kubwa ya suluba au kutumia kemikali kali.

Vifaa pekee unavyoweza wakati mwingine kuwaona wakiwa wamevaa ni glovu za mpira na viatu vinavyozuia utelezi kutegemea mazingira.

Emily anasema kwamba, kwa vile ilikuwa mara ya kwanza kuifanya kazi hii, awali alikuwa na wasiwasi kabla ya kuzoea.

Anasema alizoea baada ya kuona mteja anafurahia na kumtia moyo na hivyo kumfanya kuona kuwa kitu cha kawaida kufanya kazi katika mazingira hayo.

 “Na huwasili kazini nikiwa nimevaa nguo zangu na nifikapo mlangoni kabla ya kuingia, namuuliza mteja iwapo majirani hawatajali nikichojoa nguo nje mlangoni. Akisema hakuna noma, navua hapo hapo vinginevyo hadi niingie ndani na mlango kufungwa.

“Kisha tunazungumza kidogo na kufanya kazi nikimaliza naondoka zangu. Wakati mwingine wateja wananiletea maji ya kunywa kutuliza koo. Kamwe sikuwahi kujisikia vibaya lakini iwapo nahisi kuwapo kitu kisichofaa naweza kuondoka mara moja.”

Mkurugenzi wa Naturist Cleaners, Laura Smith anasema kampuni hiyo hutoa huduma kwa wateja wote wa kike na kiume na huajiri wafanyakazi wote wa kike na kiume.

Alianzishaje kampuni hiyo? Laura ambaye ni mkazi wa London alikuwa akiendesha kampuni ya kawaida ya usafi wa majumbani kabla ya kukutana na mwanaharakati mmoja wa uasili, ambaye alimpa wazo la kuanzisha biashara hii.

Laura ambaye kwa sasa pia hufurahia kuhudhuria matukio ya watu kutembea watupu anasema: “Sijawahi kamwe kuwa mtupu lakini ni mtu muwazi na ninapenda kujaribu vitu vipya na ndio maana nilianzisha kampuni hii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles