NA TENGO KILUMANGA,
MARA nyingi najiuliza hivi kuna ubaya duniani? Kuna roho mbaya kweli? Na kama watu wapo wenye roho mbaya ni watu wa aina gani? Na ni sababu gani zinawafanya watu wengine kuwa na hisia kama za namna hiyo? Ni kitu gani kinamfanya binaadamu mwingine kumnyima au kumzibia mtu mwingine riziki yake?
Labda haya yote si kitu cheny​e ma​ajabu, ni tabia tu ya binaadamu na hakuna kitu kibaya au kizuri, ila ni jinsi sisi bindamu tunavyotaka kutafsiri mazingira yetu na kutokana na mahitaji hayo tunatengeneza mwongozo wa jinsi jumuiya itafanya kazi na kuheshimu Maono na matakwa ya wengi.
Woni miongoni ya mambo ya msingi ambayo mara nyingi inatufanya binaadamu tunachukua uamuzi na kufanya vitendo ambavyo kikawaida viko chini ya utu na hadhi yetu. “Ukatili” ambao unakuja kwa sababu ya woga huo wa binaadamu na mambo mengine ambayo yanasababishwa na vitendo kutokana na kutokuona mbali na kwa upana vinaturudisha sana kama jamii.
Nguvu nyingi unaweka kwenye kutengeneza mpaka kuliko kutafuta njia za kuimarisha mawasiliano kwa kupanga na kujenga mikakati na miundombinu chanya na maendeleo endelevu. Nguvu ya woga ni kubwa sana katika jamii na jumuiya mbalimbali. Historia mara kwa mara imetuonyesha madhara yake na ni kitu ambacho tujaribu sana tusikiruhusu kitufanye tupotezee imani kati yetu na kujenga hisia za kutokuelewana.
Ukishuka kwenye ngazi za watu utaona kwamba ubinafsi unaleta woga na watu wana ubinafsi sana utaona ni rahisi sana watu kama hao kuwa tayari kufanya mengi kuziba riziki ya mwingine. Kujisikia woga ni kitu ambcho kinakuja kikawaida , ambacho binaadamu wote wanacho.
Kuna mstari mwembamba sana kati ya upendo na chuki, au hofu na imani. Hizi hisia zote zinafahamika na kusikiwa na watu mara kwa mara. Kitu gani kinaweza kukabiliana na hisia kama hizi na kuweza kupiga vita imani mbaya katika jamii? Kukabiliana na mawazo potofu hisia hii huleta katika jamii, ni misingi imara ambayo inaona kwa wote na kutendea haki wote.
Utamaduni mzuri, mazingira mazuri na mipango mizuri ambayo inatoa fursa kwa wote katika jamii. Katika jamii pia ni milango yote ipo wazi kwa yeyote ambao anao uwezo wa kujenga maisha yake kwa mujibu wa sheria. Hapa ni Watanzania wote wanapewa nafasi hiyo, si wa ndani tu na wale wa nje pia.
Matumaini mapya na ndoto mpya juu ya kufanya mambo mapya, kiumbe kipya kinazaliwa na kuchukua mfumo mpya katika maisha. Moyo na roho ambazo zimejaa upendo wa kutaka kuendeleza katika kuwapo kwa maongozi kufanya mambo makubwa katika maisha yetu. kubeba mbegu za vizazi vyetu siku za nyuma mchanganyiko na mseto wa Mashariki, Magharibi na Afrika. Hii ni sababu ya sisi kuwapo duniani.
Ni kwa ajili hiyo. Dunia lazimaa iendelee na ukiangalia picha yote utaona sisi si hata tone la baharini lakini mambo binaadamu wanayofanya ni makubwa kuliko binaadamu wenyewe. Dhana shirikishi ambapo maisha hayana kizuizi na miili yetu ni vyombo na kiolesura nzuri kwa hata makuu zaidi, kifaa muhimu ambacho kimetubeba na kitaendelea kutubeba tu, enzi na enzi.
Vizazi vijavyo pengine vitaelewa kwamba kuna maisha katika kila kitu na vitu vyote, na sisi ni kweli tumeungana na ni kitu kimoja, viumbe vilivyo hai au visivyo hai ni sisi sote ni yote yaliyotolewa mara kwa mara na bila kuchoka kutokana na uunganishi wetu na kuendelea kiroho katika maisha nguvu.
Nami wakati wote nitakuwa mnyenyekevu na kushukuru Mungu kwa ajili ya zawadi niliyopewa kwa mkopo kama baba na mzazi, kwa kuniwezesha kuwapa wanangu urithi wao kwa kule walikotoka na wao waweze kuwapa watoto wao, namshukuru Mungu kwa muda huu mfupi tuliopewa wa kuendeleza tulioachiwa na vizazi vilivyopita na kuwapa vizazi vyetu tunayofahamu na thamani ya nafsi kugawana nao uzoefu wa maisha yetu na kuwasaidia wawe viumbe bora kuliko sisi milele tulivyokuwa.
Hiki ni kilio cha Wanadiaspora, tusinyimwe nafasi ya kuwapa watoto wetu chanzo cha shina lao, tusinyimwe pia kuwapa wenzetu tuliojifunza na tunayoyafahamu, kwani mwisho wa siku wote tumepata.
WanaDiaspora wana mchango mkubwa sana kwenye ngazi zote…​
Ukishafahamu haya yote, basi iliyobaki ni kasi tu ya kutekeleza uliyoyalenga..