WABUNGE UINGEREZA KUANZA KUJADILI KUJITOA UMOJA WA ULAYA

0
549
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May

Wabunge nchini Uingereza waridhia kufanyika kwa mazungumzo kujadili  kujitoa katika Umoja wa Ulaya (EU)

Kati ya wabunge hao, wabunge 494 waliupigia kura muswada huo huku wengine 122 wakikataa kuupigia kura, kuweza kuiruhusu serikali ya Uingereza kuanza miaka miwili ya majadiliano ya nchi hiyo kujitoa katika Umoja wa Ulaya.

Pamoja na hilo, uamuzi huo utapelekwa katika Bunge la juu la Uingereza (House of Lords) ili kupata maamuzi ya mwisho.

Naye Waziri Mkuu Theresa May amesema anataka kuanza mazungumzo rasmi ifikapo mwishoni mwa mwezi wa tatu.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here