25.9 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

PROFESA SHIVJI AWASHANGAA VIONGOZI KUTOMZIKA CASTRO

JONAS MUSHI NA PATRICIA KIMELEMETA-DAR ES SALAAM


 

shivjiMWENYEKITI wa Kavazi la Mwalimu, Profesa Isa Shivji, amesema ni aibu kwa kiongozi wa nchi kushindwa kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa Rais wa Cuba, Fidel Castro wakati alikuwa mpigania mapinduzi wa nchi za Afrika ikiwamo Tanzania.

Akizungumza katika kongamano la kumuenzi Rais Castro jijini Dar es Salaam jana, Profesa Shivji alisema kuwa kiongozi huyo ni miongoni mwa watu walioshirikiana na viongozi wa Afrika akiwamo Mwalimu Julius Nyerere ili kuongoza mapambano dhidi ya ubeberu.

Alisema katika uhai wake, rais huyo wa Cuba alitetea masilahi ya wanyonge na kuhakikisha nchi za Afrika hazitawaliwi na wakoloni kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali akiwamo hayati baba wa taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

“Ni aibu kwa kiongozi wa nchi na watawala kushindwa kuhudhuria mazishi ya Fidel Castro. Wenzangu naona mmenyamaza lakini mimi nimeshindwa naona ni aibu kabisa kwa sababu Castrol alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha nchi za Afrika zinaweza kujitawala, Rais huyo wa Cuba alifanya kazi na Nyerere kwa karibu akisaidia elimu na afya,” alisema Profesa Shivji.

Alisema Castro alikua ni kiongozi wa pekee aliyekubali kutoa rasilimali zake kwa ajili ya kusaidia nchi za Afrika, jambo ambalo limechangia serikali ya awamu ya kwanza kupata madaktari zaidi ya 300 na walimu walioletwa kwa ajili ya kufanyakazi nchini.

Mbali na hayo kiongozi huyo aliweza kutoa mafunzo mbalimbali ya kijeshi kwa baadhi ya askari waTanzania na nchi nyingine za Afrika ili kuhakikisha wanawajengea uwezo wa kujitawala.

Aidha Profesa Shivji alitolea mfano kwa Rais wa Afrika ya Kusini, Jacob Zuma na Naibu wake ambao wamesahau harakati za ukombozi na kujilimbikizia mali.

Aliwashauri wadau wa elimu kutoa elimu kwa vijana ili waweze kujua umuhimu wa mapinduzi pamoja na waliofanikisha  harakati hizo na jinsi ya kutetea taifa lao.

Katika hatua nyingine, mwandishi mkongwe, Jenerali Ulimwengu aalisema vjana ni kioo cha taifa, hivyo wanapaswa kufundishwa siasa ili waweze kuwa viongozi bora.

Alisema hatua ya baadhi ya viongozi kupiga marufuku siasa shuleni kunachangia kurudisha nyuma harakati za ukombozi nchini.

“Mwalimu Nyerere alikuwa akifanya siasa vyuoni ili kuwapata vijana hodari ambao watakuwawana mapinduzi kwa ajili ya kutetea maslahi ya taifa lao, jambo ambalo alifanikiwa,”alisma Ulimwengu.

Kwa upande wake, Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Jorge Luis Lopez Tormo, alisema anashukuru kuona Watanzania wakijadili fikra za Castrol na kusema ni fikra zinazoweza kutumika katika vizazi vyote vya sasa na baadaye.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles